Rais Samia apiga marufuku uuzwaji holela wa mazao, azitaka Wizara kuandaa mfumo maalum

August 9, 2023 3:38 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Mfumo huo utaiwezesha Serikali kukusanya fedha na kudhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu.
  • Asema utawaisaidia wakulima kupata faida.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amepiga marufuku uuzwaji holela wa mazao yanayozalishwa nchini unaofanywa na wakulima na kuagiza wizara zinazohusika kuandaa mfumo maalum utakaosimamia mauzo ya mazao nje ya nchi.

Wizara hizo ni pamoja na Wizara ya Kilimo iliyopo chini ya Hussein Bashe, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Uhamiaji chini ya Hamad Masauni, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi chini ya Angellah Kairuki na Mamlaka ya Mapato (TRA).

Rais Samia aliyekuwa akihitimisha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, leo Agosti 8, 2023 amesema mfumo huo utaiwezesha Serikali kukusanya fedha na kudhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu.

“Tunataka tuwe na mfumo rasmi wa ununuzi, uuzaji na usafirishaji wa mazao yetu, utaratibu huo utatuwezesha kufahamu kiasi cha mazao yanayouzwa nje na fedha inayopatikana ili kudhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu,” ameongeza Rais Samia.

Mbali na kudhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu Rais Samia amesema Serikali yake itadhibiti uuzaji holela wa mazao ili kunufaisha wakulima wanaotengemea shughuli hiyo kujipatia kipato.

Kauli ya Rais Samia inakuja baada ya kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara kuzuiwa kusafirisha mazao nje ya nchi na jambo hilo limesababisha kuporomoka kwa bei ya mahindi.

Itakumbukwa Juni 22, 2023 Mbunge wa Mbozi, George Mwenisongole alimuomba Spika wa Bunge Tulia Ackson kujadili kwa dharula zuio la Serikali la kusafirisha mazao nje ya nchi jambo lililosababisha kuporomoka kwa bei ya mahindi na kufikia Sh7,000 kwa kilo 20 ambapo Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alifafanua kuwa kilichozuiwa ni usafirishaji holela wa mazao ambapo Serikali inaandaa mfumo maalumu.


Soma zaidi


Awali Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewahakikishia wakulima kuwa Wizara yake kupitia Wakala wa Uhifadhi wa Chakula imejipanga vyema kunununua mazao ya wakulima kwa bei nzuri itakayowawezesha wakulima kupata faida.

“Nataka niwahakikishie wakulima mama amefungua pochi NFRA ina fedha CPB ina fedha nendeni mkalime tutaendelea kununua mazao kwa bei competitive (shindani) ambavo itakuwa inafanya wafanyabishara waliokuwa wananunua mazao kwa Sh200 sasa wanunue kwa bei ya soko halisi,” amesema Bashe.

Katika hafla hiyo ya kilele cha sikukuu ya wakulima Rais Samia ametembelea mabanda mbalimbali ya wakulima, wafugaji na wavuvi walioshiriki katika maonesho ya sikukuu hiyo kujionea jitihada, ubunifu na maendeleo ya shughuli wanazozifanya.

Pia amezindua uchimbaji wa visima 67,850 ambapo kila kisima  kimoja kinatarajiwa kuhudumia wakulima wadogo 16 ambao pia watapewa ekari 2.5 za seti ya umwagiliaji(irrigation set). 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
28 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
29 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
29 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Lissu: Serikali haikutishwa, hivyo hakuna kosa la uhaini

Lissu: Serikali haikutishwa, hivyo hakuna kosa la uhaini

Nukta TV

Ratiba rasmi mitihani ya darasa la nne, saba na kidato cha pili na nne 2026.

Ratiba rasmi mitihani ya darasa la nne, saba na kidato cha pili na nne 2026.

Nukta TV

Wanu ataja changamoto sita, ratiba ya mitihani ya taifa yabadilika

Wanu ataja changamoto sita, ratiba ya mitihani ya taifa yabadilika

Nukta TV