Latra kuwatumia mawakala kufanikisha huduma za usafirishaji
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kupokea maoni ya wadau kuhusu rasimu za kanuni mpya za Latra kuhusu mawakala. Picha | Mariam John.
- Baadhi ya kazi zake zitafanywa na wadau wa usafiri wakiwemo madereva.
- Hiyo itasaidia kuongeza ufanisi na kuokoa muda wa kutoa huduma.
- Kanuni mpya za mawakala zinaandaliwa kufanikisha utaratibu huo.
Mwanza. Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inakusudia kuwatumia wadau wa usafirishaji wakiwemo madereva wa bodaboda kuwa mawakala wake ili kuimarisha ufanisi na muda wa utekelezaji wa majukumu yake.
Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri Wizara ya Ujenzi, sekta ya uchukuzi, Mhandisi, Aron Kisaka amesema utaratibu huo utasaidia makundi hayo kuweza kufanya shughuli za Latra na kusimamia hilo eneo walilopo.
Akitolea mfano, Kisaka amesema iwapo waendesha daladala watajiunga na kuwa na mfumo mzuri wa uongozi wataweza kufanya na wataweza kutengeneza umoja wenye nguvu utakaowasidia kuwa mawakala wa Latra.
“Kwanza watakuwa wameIpunguzia kazi latra lakini pia kulipunguzia kazi Jeshi la Polisi,” amesema Kisaka akizungumza kwenye mkutano uliokutanisha mawakala wa usafirishaji mkoani Mwanza Mei 18, 2023.
Zinazohusiana:
-
Fahamu chanzo na namna unavyoweza kutibu ‘kikwapa sugu’
-
Hiki ndicho chanzo kikuu cha maumivu ya mgongo
Amesema kupitia umoja huo pia wataweza kuanzisha vikundi vya kusaidiana kiuchumi ikiwemo Saccos zitakazosaidia kukopeshana wao kwa wao na kuwekeza katika vyombo vya usafiri.
“Haya ni mabadiliko ambayo ya kuhakikisha wanaiona sekta vizuri na kuitengeneza katika mazingira ambayo watu wataendelea kuwekeza na watakuwa na vyombo vyao vinalindwa na huduma zinakua bora na salama,” amesema Kisaka.
Amesema mabadiliko hayo wanayazingatia wakati wanaendelea kuandaa kanuni zitakazoongoza suala hilo.
Kuhusu rasimu za kanuni mpya za mawakala zilizowasilishwa kwa mawakala hao, Mkurugenzi huyo ameainisha mambo matatu yatakayowasaidia mawakala hao ikiwemo kumlinda msafirishaji mwenye kutoa huduma kwa ufanisi ili asifilisike.
Pia kuhakikisha wanapotoa huduma wanapata huduma bora na salama lakini pia kuhakikisha mapato ya Serikali yanapatikana kwa wakati.
Wakitoa maoni yao kuhusu kanuni hizo baadhi ya wasafirishaji wamesema suala la ukaguzi kwa kutumia mitandao utasababisha vyombo vingi vya usafiri kuondolewa barabarani kwa kuwa magari yanayoruhusiwa kuingia nchini mengi ni chakavu.
“Katika utekelezaji wa kanuni wakambuke na hayo ili yasilete mgogoro kwa kuwa magari mengi ni chakavu hivyo huo mfumo utasababisha magari mengi kuondolewa,” amesema Maige Lyoba, mdau wa uafirishaji.
Latest