Kutana na App inayokurejeshea ‘password’ ya simu uliyosahau

July 16, 2019 6:26 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Inakutunzia neno la siri na kukumbusha kama umesahau wakati ukitumia simu yako. 
  • Siyo rahisi kudukuliwa wala kuingiliwa na wahalifu. 
  • Pia inatumika katika utunzaji wa nyaraka muhimu mtandaoni. 

Huenda wewe ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakisahau neno la siri (Password) la simu yako au mitandao ya kijamii mara kwa mara, jambo linalokuletea usumbufu wa  kuifungua upya na kujikuta ukipoteza baadhi ya vitu muhimu. 

Basi suluhisho limepatikana, kwa kutumia programu tumishi ya Dashlane iliyotengenezwa na kampuni za Google na Apple unaweza kudhibiti maneno ya siri yote za simu yako kwa kuhakikisha neno lililosahaulika linarejeshwa. 

Siyo tu inakukumbusha na kukuwekea neno la siri la kuingilia kwenye simu yako kama umesahau,  bali inahakikisha neno unalotumia linakua imara na salama. 

Utendaji wa App hiyo unatumia mfumo wa usanifu wa maarifa sifuri (Zero Knowledge Architecture) ambapo unatengeneza neno la siri kuu ambalo linatunzwa nje ya mtandao ambapo siyo rahisi kudukuliwa au kufahamika hata kwa Wahandisi wanaosimamia app hiyo. 


Soma zaidi: 


Hata kama umedukuliwa mtandaoni, Dashlane inakujulisha mara moja kubadili neno la siri la simu, kompyuta na mitandao unayotumia ili kujiweka salama zaidi.

Unaweza pia kuitumia Dashlane katika shughuli za utunzaji wa nyaraka kwenye vifaa vingine kama kompyuta ikiwemo taarifa za risiti za mauzo, usafirishaji na hata kadi za manunuzi mtandaoni. 

App hiyo yenye watumiaji zaidi ya milioni 10 inapatikana bila malipo yoyote lakini changamoto yake ni kuwa haiwezi kufungamanishwa na barua pepe zaidi ya moja. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV