Teknolojia mpya ya kukupatia usingizi wa uhakika nyumbani
- Ni vifaa maalum vinavyopunguza sauti ambazo zinaingilia usingizi.
- Udogo wake unampatia wepesi mtu kulala nazo.
- Vinawafaa watu wenye tatizo la usingizi.
Dar es Salaam. Siyo watu wote wanaweza kulala mahala penye kelele. Wengine hata wakipata usingizi, mnong’ono wa mtu unatosha kuwakatisha kwenye usingizi wao.
Kwa lugha ya kigeni, watu hawa huitwa “light sleepers”. Mlio wa taa kuwashwa, hatua za mtu kutembea kwao zinatosha kukatisha usingizi ambao unaweza kuwa uliotumia saa kadhaa kupatikana.
Tovuti ya masuala ya afya, Medical News Today imeandika kuwa, hali ya kuwa na usingizi mwepesi inaweza kuchangiwa na hofu ambayo mtu anakuwa nayo wakati wa kulala.
“Mtu mwenye hofu akilala anaweza kuamka kwa wepesi kuliko mtu ambaye amerelax,” imeandika Medical News Today.
Wadau mbalimbali wa masuala ya kiafya wameshauri baadhi ya njia zitakazokusaidia kulala usingizi wa uhakika ikiwemo kuhakikisha chumba chako ni kisafi na kina ukimya ili kukuwezesha kupata usingizi mzuri.
Zaidi, ni kuhakikisha unalala na shuka stahiki kwani endapo shuka lako haliendani na hali ya hewa, lazima utashtuka usiku.
Hizo ni njia za awali. Kwa sasa, wataalamu wameibuka na teknolojia ambayo inaweza kupunguza sauti zote ambazo zinaweza kumfanya mtu ashtuke usingizini.
Hatua za mtu akitembea, sauti za milango kufunguliwa na kufungwa na hata sauti ya maji yakiflashiwa chooni, kwa teknolojia hiyo huwezi kuvisikia.
Vifaa hivyo ni muhimu kukupa usingizi mwanana bila usumbufu wowote. Picha| QuietOn.
“QuietOn 3 earbuds” sokoni kukupa saa nane za usingizi
Kwa mujibu wa tovuti ya afya ya Healthline, mtu mzima anatakiwa kupata saa nane za usingizi kwa siku huku watu wenye miaka 13 hadi 19 wakishaurwa kupata saa nane hadi 10 za kulala kwa siku. Lakini kwa ambao wana usingizi mwepesi, huenda hilo likawa zito kufikiwa.
Kampuni ya kutengeneza vifaa vy sauti ya Quieton imeingiza sokoni vifaa vya kumsaidia mtu kulala bila ya kukatishwa usingizi na shughuli za kimazingira.
Teknolojia hiyo inafanana na zile vifaa vya kusikiliza muziki (earbuds) lakini tofauti yake na “earphones” ni kuwa hizi hazichezi muziki na badala yake zinaondoa kelele sumbufu.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la The Verge, ‘Quieton 3 earbuds’ ni ndogo ikilinganishwa na matoleo ya awali yaani ‘QuietOn 2 na 1’.
Udogo wake unazifanya kukaa vizuri masikioni na hivyo mtumiaji kutokubugudhiwa nazo hata akiwa usingizini.
Soma zaidi:
-
Wamarekani waunda kifaa cha kuwasaidia wanaokoroma usingizini
-
Wabuni teknolojia kuzuia kelele zinazokunyima usingizi
- Jinsi unavyoweza kuishinda sonona isiharibu maisha binafsi, kazi
Usingizi unakuja vipi?
Tofauti na visaidizi vingine vya kupata usingizi mzuri ikiwemo ‘Bose Sleepbuds II’, quieton 3 hazichezi muziki wa taratibu au kumpatia mtumiaji sauti za kuliwaza ikiwemo mvua na zinginezo.
Quieton zinampatia mtu uzingizi kwa kuzuia sauti zinazosumbua usingizi ikiwemo muungurumo wa friji, feni, kiyoyozi na sauti zingine. Zimetengenezwa kumwezesha mtumiaji kusikia sauti muhimu ikiwemo “alarm” na ving’ora vya tahadhari.
Quieton 3 zinatumia kinasa sauti (mike) ambacho kinageza sauti ya kelele na kisha kuipunguza kufikia kiasi ambacho hakimsumbui mtu.
Latest
