Kisa corona, Twitter yafuta akaunti zaidi ya 170,000 za China

June 12, 2020 11:41 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Akaunti  zinazodaiwa zinauhusina na Serikali ya China.
  • Zimekuwa zikitumika kupotosha kuhusu Corona na masuala ya demokrasia.
  • Twitter yasema zilikuwa na wafuasi wachache na zinatumia lugha ya Kichina. 

Mtandao wa Twitter umetangaza kufuta akaunti zaidi ya 170,000 zenye mahusiano na Serikali ya China ikidai zimekuwa zikitoa habari mbalimbali za kupotosha ikiwemo ugonjwa wa virusi vya Corona. 

Twitter imesema katika taarifa yake iliyotolewa Juni 12, 2020 kuwa akaunti hizo pia zimekuwa zikisambaza propaganda zinazokipendelea Chama cha Ukomonisti cha China na kupinga maandamano ya raia wa Hong Kong.

Kufutwa kwa ukaunti hizo ambazo zilikuwa zinatumia zaidi lugha ya Kichina kunahusishwa na kukiuka sera za mtandao huo kwa sababu baadhi ya maudhui yake yalikuwa na viashiria vya uchochezi, ubaguzi na upotoshaji hasa ugonjwa wa COVID-19. 

Mtandao huo ulizuiwa kufanya kazi China, lakini watu wengi nchini humo wanautumia kwa mfumo wa maalum wa VPN. 


Zinazohusiana:


Kati ya akaunti zilizofutwa, 23,750 zilikuwa halali huku 150,000 zilibainika kuwa zilikuwa zinatumika kuzipa nguvu meseji ambavyo zilikuwa zinawekwa na akaunti hizo mtandaoni. 

Twitter imesema makundi hayo mawili ya akaunti yalikuwa na wafuasi wachache na muingiliano mdogo  wa watu mtandaoni. 

Kampuni hiyo ya Marekani imekuwa ikikosolewa vikali siku za hivi karibuni kutokana na sera yake ya kukaza uzi kudhibiti upotoshaji huku baadhi wakisema sera zake zinaweza kuminya uhuru wa kutoa maoni kuliko inavyodhaniwa. 

Huenda hatua hiyo ikasaidia katika mapambano ya COVID-19 ikizingatiwa kuwa baadhi ya watu hutumia janga hilo kupotosha umma. 

 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV