Kila baada ya saa 24, watoto 500 hufariki kwa ajali za barabarani

November 22, 2022 5:36 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kutokana  na sababu mbalimbali ikiwemo uzembe na kutozingatia sheria za usalama barabarani. 
  • Umoja wa Mataifa wazindua kampeni kupunguza vifo hivyo. 

Dar es Salaam. Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Usalama Barabarani (UNRSF) umesema kila baada ya saa 24 watoto 500 hufariki dunia barabarani kutokana na sababu za kibinadamu na kutozingatia sheria za usalama barabarani. 

UNRSF imeeleza zaidi kuwa mtu mmoja hufariki dunia barabarani kila baada ya sekunde 24 huku asilimia 93 ya vifo milioni 1.3 vya barabarani duniani na majeraha mabaya milioni 50 ya barabarani hutokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

UNRSF imetoa takwimu hizo Novemba 21, 2022 wakati wa uzinduzi wa toleo la pili la kampeni yake ya kimataifa ya #moments2live4 ili kuwafahamisha raia duniani kote kuhusu athari mbaya za barabara zisizo salama kwa watoto.

Mfuko huo umetoa wito wa michango ya mtu binafsi kusaidia lengo la Dola za Marekani milioni 40 (Sh93.3 bilioni) ili kusaidia kupunguza vifo vya watoto wanaokufa kwa ajali za barabarani. 

“Uhamasishaji ni hatua ya kwanza kuelekea kukabiliana na changamoto ya kimataifa ya usalama barabarani. Mabilioni ya watumiaji wa barabara kila siku, maelfu ya mashirika na zaidi ya serikali 100 kwa sasa wako katika upande wa kutochukua hatua, kwa kiasi kikubwa hawajui hatari kubwa kwa watumiaji wetu wa barabara walio hatarini zaidi – watoto wetu,” imesema UNRSF.

Imesema kampeni yake inakusudia kumwezesha kila mtu kupata ujuzi kuhusu jinsi ya kusaidia kuwaweka watoto salama barabarani. 

Nneka Henry, Mkuu wa UNRSF amesema kuwa, “kwa msaada kutoka kwa waungaji mkono mbalimbali tunatumai kampeni hii itaanzisha msaada wa ziada kwa mamlaka ya mfuko na kufanya kazi katika nchi zinazoendelea.” 

Kampeni ya kimataifa ya #moments2live4 inashirikisha watu mbalimbali kuanzia kwa madereva wa magari za mashindano; watumbuizaji, wanariadha wa kiwango cha kimataifa, na viongozi wa dunia kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa baada ya kujifunza kuhusu athari za barabara zisizo salama na matumizi mabaya ya barabara kwa watoto. 

Waungaji mkono kadhaa wa kampeni hii wanajivunia mtandao wa pamoja wa hadi wafuasi milioni 50 wa mitandao ya kijamii, ambao utakuwa muhimu sana katika kukuza umuhimu wa suala hilo miongoni mwa mamilioni ya familia ambazo huenda hazikuwa na ufahamu wa kutosha. 

Kampeni hiyo itaendeshwa kwa wiki 10 hadi Siku ya Kimataifa ya Elimu Januari 24, 2023. 

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA AKIHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU, UONGOZI DARAJA LA PILI KOZI 2025/26

🔴LIVE: RAIS SAMIA AKIHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU, UONGOZI DARAJA LA PILI KOZI 2025/26

Nukta TV

Rais Samia: Anzisheni mfuko  kuwasaidia wafungwa wenye ujuzi wanapotoka gerezani

Rais Samia: Anzisheni mfuko kuwasaidia wafungwa wenye ujuzi wanapotoka gerezani

Nukta TV

🔴LIVE: RAIS SAMIA AKIHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU, UONGOZI DARAJA LA PILI KOZI 2025/26

🔴LIVE: RAIS SAMIA AKIHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU, UONGOZI DARAJA LA PILI KOZI 2025/26

Nukta TV