Kila sekunde 24 mtu mmoja hufariki kwa ajali ya barabarani

January 3, 2022 4:21 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Hiyo ni sawa na watu 72 kwa siku nzima ya saa 24.
  • Serikali zatakiwa kuongeza uwajibikaji katika kuimarisha usalama barabarani.

Dar es Salaam. Kama bado unachukulia poa kuhusu usalama barabarani na uendeshaji vyombo moto usiozingatia sheria, fahamu kuwa wewe ni sehemu ya kusababisha vifo vinavyotokana na jali za barabarani 

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN), kila sekunde 24 mtu mmoja anafariki dunia katika ajali ya barabarani. Hiyo ina maana kuwa watu takribani watatu katika dakika moja na jumla ya watu 72 kwa siku nzima ya saa 24 wanafariki kwa ajali za barabarani.

Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres katika maadhimisho ya siku ya kukumbuka waliopoteza maisha au kujeruhiwa kutokana na ajali za barabarani yaliyofanyika jana Novemba 21, 2021 amesema ni wakati wa kutafakari juu ya vifo vilivyosababishwa na ajali za barabarani.

“Mwaka huu maudhui yanamulika umuhimu wa kupunguza mwendokasi barabarani ili kuzuia vifo na majeraha, hususan miongoni mwa vijana wa kike na wa kiume,” amesema Guterres akibainisha kuwa “pia waenda kwa miguu na watu wenye ulemavu.”

Guterres anatoa wito kwa kila nchi, kampuni na raia kusaidia juhudi za kitaifa na kimataifa za kuhakikisha barabara zinakuwa salama zaidi hususan katika nchi za kipato cha chini na kati ambako zaidi ya asilimia 90 ya vifo vitokanavyo na ajali barabarani hutokea.

Amezitka pia nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuridhia mikataba ya kimataifa ya usalama barabarani na kutekeleza mipango kazi yote ya utekelezaji.

Kwa wahisani, ametoa wito waimarishe michango yao ya kifedha na kiufundi kupitia mfuko wa Umoja wa Mataifa wa usalama barabarani.

“Tunapotazamia mkutano wa mwaka ujao wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mbinu za kuimarisha usalama barabarani, hebu na tukumbuke kuwa kila mmoja wetu ana jukumu la kufanya ili barabara zetu ziwe salama. Leo na kila siku tuazimie barabara ziwe salama kwa kila mtu kokote aliko,” amesisitiza Guaterres.

Siku ya kukumbuka waliokufa au waliojeruhiwa kutokana na ajali za barabarani inatokana na azimio namba 60/5 la Desemba  Mosi mwaka 2005 lililopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, huku mwaka 2020 Umoja wa Mataifa ukitangaza muongo mmoja wa kuimarisha usalama barabarani kuanzia mwaka 2020 hadi 2030.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV