Kila baada ya dakika 1 watu 2 wanafariki kwa ajali za barabarani

July 2, 2022 7:49 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Hiyo ni sawa na takriban watu milioni 1.3 ambao hupoteza maisha kila mwaka.
  • Sababu za kibinadamu huchangia kwa sehemu kubwa ajali hizo.
  • WHO yawataka wadau kubuni njia mpya kumaliza ajali hizo.

Dar es Salaam. Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kila baada ya  dakika moja, watu wawili duniani hupoteza maisha  kutokana na ajali za barabarani ambapo asilimia 90 ya wahanga hao wanatoka katika nchi zinazoendelea.

WHO katika chapisho lake lililotolewa Juni 28 hiyo ni sawa takriban watu milioni 1.3 ambao hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ajali za barabarani. 

Chapisho hilo linafafanua zaidi kuwa licha  ya vifo hivyo, ajali za barabarani hujeruhi watu milioni 50 kwa mwaka, huku zikihusisha watembea kwa miguu na watumia baiskeli.

“Kifo kimoja kati ya vinne vinavyotokea kutokana na ajali za barabarani kinamuhusu mtembea kwa miguu au mwendesha baiskeli,” imeeleza WHO.

Ajali za barabarani nchini Tanzania zapungua

Mbali na takwimu za jumla za ajali za barabarani, Tanzania inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha inapunguza ajali za barabarani ili kunusuru maisha ya wananchi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Uhalifu na Makosa ya Usalama Barabarani za ya mwaka 2020 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Jeshi la Polisi, ajali za barabarani zimepungua kutoka 2,704 mwaka 2019 hadi ajali 1,714, zilizotokea mwaka 2020.

Ajali hizi zimepungua kwa asilimia  39.6, huku Zanzibar ikiwa na ajali 219 kwa mwaka 2020 ambapo kwa asilimia 0.5.


Zinazohusiana:


Ajali za barabarani zilizotokea kwa mwaka 2020 nchini  zimesababisha vifo vya watu 1,384 na majeruhi 2,362.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa sababu za kibinadamu ndio chanzo kikubwa cha ajali za barabani ambapo asilimia 91 zinatokana na chanzo hiki, huku uzembe wa madereva na mwendo kasi vikitajwa kuchangia vifo hivyo.

Sababu nyingine iliyotajwa ni  ubovu wa vyombo vya usafiri  unaohusisha hitilafu za magari barabarani, sababu za kimazingira zikiwemo moto, vivuko vya reli na ubovu wa barabara.

UN yajipanga kupunguza nusu ya ajali za barabarani ifikapo 2030

WHO kwa kushirikiana na wadau wengine wa usalama barabarani,  wameandaa mpango wa dunia wa karne ili kuchukua hatua za usalama barabarani, ambao utaweza kupunguza ajali za barabarani kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

Mpango huo unatoa wito kwa serikali na wadau wote kuchukua njia mpya, ambayo itaokoa maisha na kuzuia majeraha, Ili kuzuia  athari za kiuchumi za majanga yatokanayo na ajali yanayoweza kuzuilika.

Sambamba na hilo pia waimeitisha  mkutano  wenye kaulimbiu isemayo  “Kuufikia mwaka 2030 kwa ajili ya usalama barabarani: kupata muongo wa utekelezaji na utimizaji”.

Mkutano huo una lengo la kukaribisha tamko la siasa au azimio litakalopitishwa na nchi wanachama wa UN, li kuimarisha usalama wa barabarani.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV