Mambo ya kufahamu kuhusu ajali za barabarani duniani

January 2, 2023 11:28 am · admin
Share
Tweet
Copy Link

  • Asilimia 90 ya ajali hutokea katika nchi zinazoendelea au zenye uchumi wa kati.
  • watu wenye umri miaka 15-19 ndio wanaongoza kwa kupoteza maisha.

Dar es Salaam.  Ajali za barabarani huenda zikawa chanzo cha saba kikuu cha vifo duniani ifikapo mwaka 2030 kama hazitafanyika jitihada za dhati katika kudhibiti ajali zinazoendelea kutokea hasa katika nchi masikini au zenye uchumi wa kati.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) takribani watu milioni 1.2 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ajali za barabarani na watu wenye umri wa miaka 15 hadi 29 ndiyo walio kwenye hatari zaidi ya kupoteza uhai au kujeruhiwa kutokana na ajali hizo.

Kwa mujibu wa Takwimu za Hali ya Uhalifu nchini Tanzania kati ya Januari hadi Disemba mwaka 2020 zaidi ya watu 1,200 walipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani.

WHO wanaonya kwamba ajali za barabarani huathiri ukuaji wa pato la taifa kwa asilimia 3 kwa nchi zinazoendelea.

Enable Notifications OK No thanks