Jinsi vijana wanavyoweza kuachana na tabia hatarishi

May 24, 2021 5:58 am · Neema
Share
Tweet
Copy Link
  • Baadhi ya tabia zinafananishwa na ulevi kwa sababu zinaharibu maisha ya mtu.
  • Njia ya kuzishinda tabia hizo kufahamu tatizo liko wapi na kuanza kujielekeza katika mambo yenye manufaa. 

Dar es Salaam. Wengi wetu tumezoea kuona watu wakinywa pombe kwa kupitiliza na tunawaita walevi. Lakini hatufahamu kuwa ulevi ni zaidi ya kunywa pombe.

Huenda watu wote ni walevi lakini wanatofautiana katika mambo yanayowafanya walewe na kufanya baadhi ya mambo kwa kupitiliza na kuathiri maisha yao ya kawaida.

Wewe ulevi wako uko katika nini? Wapo ambao wanatumia simu kupita kawaida, kucheza michezo ya mtandaoni, kupenda mpira, kamali na hata kupiga umbea na bado wakasema wao siyo walevi. 

Siyo vibaya kufanya unachokifanya lakini una kiasi nacho au ndiyo kimekufanya ushindwe kufanya mambo mengine na kutumia muda mrefu kukifanya huku kikurudisha nyuma katika mchakato wa kujenga maisha bora. 

Mtu anapokuwa mlevi wa jambo hujikuta anashindwa kujizuia na lile  jambo  ama hicho kitu kinakuwa sehemu ya maisha yake na anaweza  akawa anajua ama hajui kabisa maana ni kawaida mwili umezoea na akili imezoea na maisha yake ndiyo yalivyo na watu waemzoea hivyo.

Bado una nafasi nzuri ya kuachana na ulevi wako na ukarejea katika maisha ya kawaida. Hatua ya kwanza, fahamu kuwa una ulevi yaani kuna tatizo. 

Tafuta mbinu au njia mbadala zitakazokufanya kuchukia jambo unalofanya sasa na anza kujielekeza katika masuala ya msingi yenye faida kwako.

Inaweza kuwa ngumu kuachana na hiyo tabia lakini ukidhamiria kwa dhati unaweza kubadilika. Tazama video hii kujifunza zaidi:

                                  

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV