Unavyoweza kujifunza kutokana na maumivu yako

September 16, 2021 10:24 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Usikimbie maumivu yako badala yake jifunze kutoka kwayo.
  • Jisamehe na jiulize njia bora zaidi za kukabiliana nayo.
  • Yafanye maumivu kuwa njia bora ya kujiimarisha.

Dar es Salaam. Mara nyingi pale tunapopitia maumivu kwenye maisha, tunasahau kitu kikubwa nyuma ya maumivu hayo. Kujifunza.

Licha ya kuwa ni hisia ambazo zinachoma moyo na muda mwingine kudondosha machozi machoni petu, hisia hizo ni maalum kwa ajili ya kutujenga na kutufunza mambo mbalimbali.

Maumivu yanaweza kutokana na vitu mbalimbali ikiwemo wazazi, mafanikio, mapenzi na wakati mwingine elimu.

Huenda mtu uliyehisi ndiye ameumbwa kwa ajili yako amekuacha au umefeli darasani na jamii imekukataa. Hizo ni baadhi ya hali zinazoweza kukuumiza kiasi cha kutamani walimwengu wote wapotee dunia ibaki yako na malaika tu.

Hata hivyo, badala ya kuomba dunia ipasuke au kuanza kujutia kuzaliwa, ni heri ukafahamu kuwa maumivu yako yanakuja kwa ajili ya kukuacha ukiwa mpya tofauti na jana. Inawezekanaje?

Unapokuwa kwenye maumivu, fanya maumivu hato kama ngazi ya kuwa bora kuliko jana. Picha| VOA.

Chagua kukua badala ya kuhuzunika

Kama muumba wetu angelitupatia kuchagua kati ya kuwa na maumivu au raha, bila shaka bustani ya wasiotaka maumivu maishani ingejaa.

Lakini wadau mbalimbali wa masuala ya saikolojia kikiwemo kituo cha masuala ya ujauzito (Pregnancy Option Centre) cha Uingereza kimeandika kuwa maumivu yanatakiwa kuwa sababu ya ukuaji wako kifikra, kimtazamo na hata kiuzoefu.


Maumivu ni chanzo cha busara zako

Fikiria hili, una maisha mazuri tu kila siku na wala hauna changamoto yoyote. Bila shaka ni maisha ambayo hayana uhai kwa sababu maisha hayo hayawezi kukufanya uwe bora zaidi.

Msaikolojia wa nchini Marekani, Tal Ben-Shahar ameandika kupitia tovuti ya Wholebeing Institute kuwa milima na mabonde ya kwenye maisha ndiyo hutuimarisha kama wanadamu na inachangia kukufanikisha zaidi kuliko maisha ya tambalale.

Ukiwa nacho utajua thamani yake kwani awali ulikuwa hauna. Inaweza kuwa imani, mafanikio, heshima na uaminifu.

Maumivu yatakupatia ujasiri na mafunzo hautayasahau. Picha| iStock.

Ufanye nini unapokuwa kwenye maumivu?

Baadhi huchagua kuyapotezea maumivu yao na kusonga mbele lakini wanasaikolojia mbalimbali wanashauri kupata muda wa kuyahisi maumivu yako.

Mkufunzi wa masuala ya ujuzi, Webster Tsenase, ameandika kuwa kushughulika na maumivu yako itakuchochea kuwa bora zaidi.

Tsenase amesema, ni muhimu kujifunza kujisamehe pale unapohisi umejikosesha kitu fulani au umefanya kitu kibaya, pambana na changamoto zako ana kwa ana badala ya kuzikimbia na pia, yasome maumivu yako.

“Ni rahisi kumshinda adui ambaye mbinu zake za upambanaji unazijua na unaweza kuzitabiri. Pitia upya maumivu yako na jiulize maswali yanayokukosesha raha ikiwemo kama ungeweza kufanya vyema zaidi,” ameandika Tsenase.

Fahamu kuwa, hakuna binadamu ambaye ameumbiwa furaha tu. ongea na watu, utashangaa kiasi cha maumivu waliyo nayo. Tengeneza furaha yako mwenyewe.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV