Polisi Tanzania wachunguza madai ya kutekwa Polepole

October 6, 2025 2:52 pm Ā· Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Lasema bado linamsubiri aripoti katika ofisi ya DCI.

Arusha. Jeshi la Polisi Tanzania limesema linachunguza madai ya kutekwa kwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, siku moja baada ya ndugu zake kueleza kuwa ametekwa na watu wasiojulikana.

Habari za kutekwa kwa Polepole, ambaye amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kukosoa mwenendo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Serikali, zilianza kusambaa Oktoba 6 asubuhi baada ya moja ya ndugu zake kueleza taarifa hizo mtandaoni.

Katika taarifa yake kwa umma, Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema bado wanaendelea kumsubiri aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Ndani ya miezi mitatu ya hivi karibuni, Polepole amekuwa akiikosoa vikali Serikali kwa nyakati tofauti hatua iliyowafanya polisi kumtaka kufika ofisini kwa DCI ili kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo.

Mmoja wa ndugu zake Godfrey Polepole ameliambia Shirika la Habari la Uingereza (BBC Swahili) kuwa walijulishwa na mwenye nyumba kuhusu iwapo wanajua tukio lilotokea nyumbani kwa Polepole.

Godfrey amesema wamekuta damu nyingi nyumbani kwa Polepole na tayari wamesharipoti tukio hilo katika kituo cha polisi Mbweni.

ā€œJeshi la Polisi limeona taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na ndugu zake kuwa ametekwa, tayari tumeanza kufanyia kazi taarifa husika ili kupata ukweli wake,ā€ amesema Misime, leo Oktoba 6, 2025.

Polepole alitangaza kujiuzuru katika nafasi yake ya ubalozi Julai 13 mwaka huu kwa madai ya kukiukwa kwa misingi ya haki.

Wiki chache baadae Rais Samia alitengua rasmi uteuzi wa balozi huyo kupitia barua rasmi ya Balozi Dk Moses Kusiluka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Habari hii imeboreshwa na kuongezwa muktadha zaidi

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Aug, 2026 Ā· TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Aug, 2026 Ā· TZS
No gainers today
No losers today
16 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV