ICJ: Urusi isitishe mara moja mashambulizi Ukraine

March 17, 2022 12:04 pm · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Mahakama ya haki ya Umoja wa mataifa yaitaka Urusi kusitisha operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine.

Dar es Salaam. Mahakama ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki (ICJ)  katika uamuzi wake uliotolewa Machi 16, Hague nchini Uholanzi imesema Urusi isitishe operesheni zake za kijeshi nchini Ukraine.

Uamuzi wa Mahakama hiyo unafuatia ombi la Ukraine la Februari 27 la kuishutumu Urusi kutumia kisingizio cha mauaji ya kimbari kuhalalisha uvamizi wake wa kijeshi nchini humo.

Majaji 13 kati ya 15 wa mahakama hiyo wameunga mkono ombi la Ukraine kutaka Urusi isitishe operesheni zake, huku majaji wawili, Makamu wa Rais wa ICJ Kirill Gevorgian kutoka Urusi  na Jaji Xue Hanging  kutoka China wakipinga ombi hilo.

Hata hivyo, majaji wote walikubaliana kuwa pande zote kwenye mzozo huo zijizuie kufanya kitendo chochote kinachoweza kuchochea zaidi mzozo wa sasa au kufanya hali kuwa ngumu zaidi kupata suluhisho.

Katika ombi lake, Ukraine ilieleza kuwa baada ya madai ya uongo ya vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa maeneo ya Luhansk na Donetsk , Urusi ilitangaza na kutekeleza operesheni maalum za kijeshi ili kuzuia adhabu dhidi ya madai yake hayo.


Zinazohusiana: 


Akiwasilisha uamuzi wa mahakama, Rais wa ICJ Jaji Joan Donoghue amesema mazingira sahihi yalikidhi kuipatia mahakama mamlaka ya kutoa uamuzi.

Jaji huyo ameeleza kuwa haki zilizosisitizwa na Ukraine zina mashiko na hakuna mauaji ya kimbari yaliyotekelezwa.

“Bila shaka, operesheni yoyote ya kijeshi, hususan inayofanyika katika kiwango kinachotekelezwa na Urusi kwenye eneo la Ukraine, inasababisha vifo, inaleta madhara ya mwili na akili, na inaharibu mali na mazingira,” amesema jaji huyo.

Donoghue ameongeza kuwa  ICJ inaona kuwa wananchi wanaoathiriwa na vita vya sasa ni wale walio hatarini zaidi.

“Uvamizi wa Urusi umesababisha vifo vya mamia ya rai na wengine wamejeruhiwa, mali zimeharibiwa ikiwemo uharibifu wa majengo na miundombinu,” amesema.

Mahakama pia imesema kuwa Urusi imekataa kushiriki kwenye mchakato wa kesi hiyo na baadaye iliwasilisha nyaraka kwa kesi hiyo kuwa  ICJ inakosa mamlaka na uhalali wa kuisikiliza na hivyo kuitaka mahakama ijizuie kushiriki katika kutoa uamuzi wowote na iondoe shauri hilo mahakamani.

Uamuzi ICJ ni wa kwanza kutolewa na mahakama hiyo  tangu Urusi ivamie Ukraine Februari  24, japokuwa uamuzi huo una mashiko, ripoti zinahoji iwapo Urusi itazingatia uamuzi huo, na Mahakama hiyo haina njia ya moja kwa moja ya kuutekeleza.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.