Huduma ya ‘Malipo ya Pasipoti kwa M-Pesa’ yazinduliwa Dar

July 17, 2019 7:58 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Inawawezesha wateja wa Vodacom Tanzania kulipia malipo ya hati za kusafiri kwa kutumia simu za mkononi zilizounganishwa na huduma ya M-Pesa. 
  • Itapunguza foleni na kuwezesha malipo kufanyika kwa haraka na urahisi zaidi. 

Dar es Salaam. Huenda Watanzania wakaondokana na usumbufu wa kukaa muda mrefu katika foleni ya malipo ya pasipoti baada kuwekewa huduma ya kidijitali unayorahisisha malipo wakiwa sehemu yoyote Tanzania. 

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji nchini wamezindua huduma mpya iitwayo ‘Malipo ya Pasipoti kwa M-Pesa’ inayolenga kuwawezesha wateja wa kampuni hiyo kufanya malipo kwa haraka na urahisi zaidi. 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa M-Commerce, Epimack Mbeteni amesema huduma hiyo mpya inalenga kuwaondolea usumbufu wateja wake kupanga foleni kwa ajili ya kufanya malipo yanayowezesha kupata hati hizo za kusafiria. 

“Ili mteja aweze kulipia inabidi aingie kwenye menu ya M-Pesa na kufuata utaratibu wa kulipa malipo ya Serikali au kupitia zana (app) ya M-Pesa. 

“Lengo letu ni kuhamasisha Watanzania wapate hati mpya za kieletroniki lakini pia kuwasogezea huduma za malipo viganjani kwao, ndiyo maana tumeona umuhimu wa kushirikiana na Uhamiaji kufanikisha hili,” amesema Mbeteni.


Zinazohusiana: 


Amesema wanaendeleza nia ya kuibadili Tanzania kuwa jamii inayofanya malipo kidijitali kwa kuwekeza katika teknolojia ya simu ambayo itaingiza watu wengi zaidi katika mifumo ya kifedha na hatimaye kufikia malengo ya kijamii na kiuchumi ya nchi.

Pasipoti za kielektroniki zinatajwa kuwa ni salama zaidi kuzitumia kwa sababu zimeunganishwa na mifumo ya usalama mtandaoni, jambo linalofanya iwe vigumu kwa mtu kuiba au kughushi taarifa za mtumiaji zilizopo katika kanzi data (data base).

Kamishna wa Pasipoti wa Uhamiaji, Marry Palmer amesema wana furaha kuungana na Vodacom Tanzania kuwawezesha wateja kufanya malipo kirahisi, vile vile kuiwezesha idara ya Uhamiaji kufanya kazi kwa urahisi zaidi. 

“Nategemea kuona bunifu nyingi zaidi kutoka Vodacom,” amesema Palmer.

Vodacom imedhamiria kuifikia idadi kubwa ya watu ambao hawapo kwenye mifumo rasmi ya kifedha, kuchochea ujumuishwaji, na uwezeshaji kupitia huduma rafiki na salama ambapo hiyo ni moja ya njia ya kufanikisha lengo hilo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV