Halmashauri zaagizwa kutunza maeneo ya kihistoria Tanzania

February 27, 2021 7:35 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Hiyo itasaidia kizazi cha sasa na kijacho kufahamu kwa undani historia ya Tanzania.

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa ameziagiza Halmashauri zote Tanzania kuhakikisha kuwa maeneo yote ya kihistoria yanatunzwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

“Natoa maagizo kwa Halmashauri zote za mkoa wa Ruvuma na halmashauri zote nchini, zitunze maeneo haya ya Urithi wa Ukombozi na mimi nitaenda kila Halmashauri kuhakikisha maeneo kama haya tunayatunza na kuyahifadhi,” amesema Bashungwa.  

Waziri Bashungwa yupo mkoani Ruvuma kwenye ziara ya kikazi ambapo Februari 26, 2021 ametembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Afrika katika Wilaya ya Tunduru kata ya Masonya mkoa wa Ruvuma.

Amelitaja eneo la Masonya kuwa limesheni utajiri mkubwa wa historia ya Tanzania na namna Tanzania ilivyoshiriki katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika.

Maeneo hayo ya kihistoria ni rasilimali muhimu kwa shughuli za utalii ambazo zinaweza kuwavutia watalii wanaopenda kujifunza historia ya Tanzania. 


Zinazohusiana:


Katibu Tawala wa Wilaya ya Tunduru Mwajuma Nasombe amesema mwaka 1966 Tanzania iliwapokea  wapigania uhuru wa Msumbiji na kuwakabidhi eneo la Masonya lililopo kilomita 16 kutoka Tunduru mjini.

Amesema hivi sasa eneo hilo limebaki kama eneo la makumbusho ambapo ametaja urithi unaopatikana katika eneo hilo kuwa ni nyumba mbili za viongozi wa kitaifa hayati Samora Machel Rais wa kwanza wa Msumbiji na nyumba aliyokuwa anafikia baba wa Taifa hayati Julius Nyerere.

Nasombe ameutaja urithi mwingine kuwa ni jengo moja la mawasiliano alilokuwa anatumia Rais Machael, ukumbi wa semina aliokuwa anatumia Machel kutoa mafunzo mbalimbali na majengo 11 ambayo kwa sasa ni madarasa ya wanafunzi wa sekondari ya wasichana Masonya.

“Maeneo mengine ya urithi ni mahandaki yaliyotumiwa na wapigania uhuru wa Msumbiji, eneo la bendera ya Frelimo na eneo la mnara ulipofanyika mkutano wa wanawake wa Msumbiji tarehe 17 Machi1973,” amesema Nasombe.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV