Filamu ya The Squid Game: Tamaa mbele mauti nyuma

October 1, 2021 1:12 pm · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayohusu mchezo unaohatarisha maisha.
  • Huku washiriki wengi wakiwa ni wadaiwa sugu.

                                   


Dar es Salaam. Katika maisha yako ulishawahi kufika hatua ambayo maisha yamekupiga ukachoka na kuchakaa kiasi kwamba lolote litakalokuja mbele yako utalifanya ilimradi tu likupatie walau ugali wa siku?

Basi filamu ya ‘The Squid Game’ inakukutanisha na watu wanaofanya maamuzi magumu baada ya maisha yao kutokuwa na ahueni kila uchao, huku mmoja wapo akiwa ni Gi-Hun.

Hun ni mhusika mkuu katika filamu hii, ambaye maisha yake amekuwa akiyaendesha kwa ‘kuunga unga’ tu, huku kazi yake kubwa ikiwa ni kucheza kamali.

Licha ya kuwa mchezo huo ni haramu walau ulikuwa unampa pesa za kuzogeza maisha mbele, kumuuguza mama yake na kumlea binti yake kipenzi. Changamoto ni kuwa mchezo huo unamzidishia Hun madeni kila siku.

Hapo kwenye madeni sasa ndiyo ‘patamu’.  Hun alipata wanaojua kudai haswaaa, na kwa wale waliowahi kukopa basi wanajua adha ya kupata wadai ambao wanakufanya utamani kuhama sayari.

Hali hiyo ndiyo ilimfanya Hun kuchukua maamuzi magumu ambayo baadaye yanamfanya kujuta. Ni  maamuzi gani hayo? 

Maamuzi ya kuhatarisha maisha 

Madeni yanapozidi Hun anaamua  ’liwalo na liwe,’ anajiunga katika mchezo ambao maisha yake yanakuwa hatarini, bora angebaki kupambana na wadai wake.

Hun anaungana wenzie 455, ambao maisha yao mtaani yamekuwa magumu mno, huku wengi wao madeni yakiwa yamewazonga kila kona kama Hun.

                             

Watu hawa wanaalikwa kwenda kucheza mchezo ambao unawatenga kabisa na jamii zao ili kuepukana na matatizoi yanayowakabili.

Cha kuvutia zaidi ni  kiasi cha pesa ambacho mshindi ameandaliwa. Ni sh88.7 bilioni. Hata ungekuwa wewe ungeanzaje kuacha ‘mkwanja’ mrefu kiasi hicho?. 

Lakini, wahenga hawakukosea waliposema tamaa mbele mauti nyuma, kwani pesa ni ndefu ila hadi uzipate shughuli yake sio ya kitoto.

Ugumu na hatari ya mchezo huo unawafanya washiriki wasizingatie tena pesa, bali kupigania maisha yao, kwani kuuwawa katika mchezo huu ni kama kupiga mhayo tu huku sintofahamu ikitanda ni lini mchezo huo utaisha ili warudi kwenye maisha yao ya zamani ambayo walau yaliwapa nafasi ya kuwa hai.

Kuuana kikatili, kuchomana moto na hata kudanganyana ni sehemu ya filamu hii, unapitwaje?

Unaweza kuitazama The Squid Game kupitia majukwaa mbalimbali ya mtandaoni ikiwemo Netflix.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV