Mfahamu ‘single mother’ mpambanaji wa filamu ya Maid

October 15, 2021 1:03 pm · Herimina
Share
Tweet
Copy Link

Licha ya kuwa vyoo vingine kuwa vichafu mno, Alex hakuacha kazi ya kufanya usafi. Picha| Stylist.


  • Ni filamu inayomuhusu Alex anayepambana ili kumlea mtoto wake.
  • Anaachana na mzazi mwenzie kwa sababu ya ukatili wa kijinsia.
  • Usafi wa vyoo ikiwa ni moja kazi yake ya kujipatia kipato.

Dar es salaam. Kwanini tu usiondoke? Ni swali alilokuwa akijiuliza Alex baada ya kupata manyanyaso kutoka kwa mzazi mwenzie Sean. Alikuwa akimtukatana, kumpiga na hata kumrushia vitu vya hatari kama chupa. kiufupi yalimfika shingoni.

Kitu kibaya zaidi ni kwamba Sean alikuwa akimfanyia yote hayo Alex mbele ya binti yao Maddy mwenye miaka miwili tu.

 Manyanyaso yalikuwa yamemchosha Alex hakuona sababu ya kuendelea na mahusiano ya vurugu kila uchao. Kuokoa jahazi, anaamua kuondoka na mwanaye tena akiwa na begi tu la nguo bila kujua ni wapi wataenda kuishi na watakula nini.

Maisha haya ni mapya kwa Alex, kuwa ‘Single mother’ (wanawake ambao wametalakiana na waume zao) siyo jambo rahisi, majukumu yote ya kumlea mtoto yapo mabegani mwake huku akiwa hana mtu anayemsaidia.

Clean Bandit hawakukosea walipoimba kibao Cha Rockabye, ambacho kinaelezea jinsi single mothers wengi wanavyopambana kwa hali na mali ili kuwalea watoto wao.

Kwa Alex pia ilikuwa hivyo hivyo. Licha ya kuwa na umri wa miaka 23 tu, jukumu la kuwa mama linamfanya kuwa tayari kufanya chochote  ili mradi apate kipato cha kumtunza mwanaye.

Shughuli ya kutafuta kibarua inakuwa ni nzito kwa Alex huku akijishikiza sehemu ya kulala kwa rafiki yake na ndipo anapokuja kuwa mfanya usafi katika sehemu mbalimbali ikiwemo vyoo vya umma. 

Alex akiwa na binti yake Maddy. Picha| Vulture. 

Safari ya milima na mabonde

Kibarua cha kufanya usafi si  mchezo, hasa katika vyoo vya umma, najua hata wewe utakuwa ni shahidi ni kwa jinsi gani vyoo vingi vya umma au kibongo bongo vinajulikana.  Kama vyoo vya kulipia vinavyokuaga vichafu, kiasi vikakufanya uhailishe hata kujisaidia.

Basi, Alex alikuwa akishinda navyo kila siku akisugua na kudeki, licha ya kuwa kuna vingine vilikuwa vichafu mno hadi kumsababishia kutapika, Alex hakuthubutu kuacha kazi hiyo, kwani alijua kuna mtoto anamtegemea.

Kazi anayofanya Alex haikutosha kumpatia fedha ya kupangisha hata chumba kimoja cha kuishi na mwanae, hivyo kila siku maisha yao yakawa ya kutangatanga katika nyumba za marafiki na ndugu.

Mbali na magumu hayo ya kimaisha anayoyapitia Alex, manyanyaso aliyowahi kupitia kutoka kwa mzazi mwenzie yanamharibu kisaikolojia  na kumfanya asiweze kulala usiku kwa ndoto alizokuwa akiota za kupigwa na kutukanwa.

Atafanya Nini Alex? Hata pesa ya kwenda kumuona mtaalamu wa masuala ya kisaikolojia hakuwa nayo, ukizingatia  fedha anazopata katika shughuli ya usafi hazikutosha hata kumnunulia mwanaye chakula kizuri au kumpeleka sehemu za kufurahi kama watoto wengine.

                                 

Maisha yanapoendela Alex, anapata udhamini wa kwenda kusoma chuo kikuu, kwani hakuwa na uwezo wa kujiendeleza kimasomo, tunaweza kusema ni bahati njema, lakini kiuhalisia majukumu ndiyo yanazidi kuongezeka.

Alex inabidi ajigawe kufanya shughuli za shule, kumlea mtoto huku bado aendelee kutafuta pesa kwa ajili ya mwanaye na pesa za chakula akiwa chuoni.

Je , maisha ya tabu na huzuni ya Alex na mwanaye yatapata ahueni siku moja? Jibu lipo katika filamu hii ya ‘Maid’ na ukiitazama utaguswa sana na kupata picha vile ‘single mothers’ wanavyopitia magumu ili mradi tu watoto wao wapate walau chakula.

Unaweza kuitazama Maid kupitia majukwaa mbalimbali ya kuangalizia filamu mtandaoni ikiwemo Netflix.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
14 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV