Diamond, Nandy kuiwakilisha Tanzania tamasha la Afrika Mei 25

May 21, 2020 7:21 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Wasanii hao wataungana na wenzao wa nchi za Afrika kushehereka siku ya bara hilo.
  • Tamasha hilo litafanyika mtandaoni kuonyesha umoja wa Afrika dhidi ya janga la Corona.
  • Unaweza kufuatilia mubashara kwenye mtandao wa Youtube au kwenye chaneli ya MTV.

Dar es Salaam. Ni nini maana ya Afrika kama siyo watu wake? Ndiyo! ngoma za kitamaduni, mavazi na sauti zenye mitetemo ya Kiafrika ndiyo Afrika yenyewe.

Tumeshuhudia matamasha mengi ya mtandaoni lakini ni kweli halikuwepo lile linalokonga Uafrika. Na sasa, limepata nafasi.

Tamasha hilo ambalo linatarajiwa kufanywa kwa njia ya mtandao Siku ya Afrika(Africa Day) Mei 25, 2020 linalenga kuliweka bara hilo katika nafasi moja ya ushirikiano hasa kipindi hiki cha mlipuko wa janga la Corona. 

Shoo hiyo (#IAmWAN) itakayodumu kwa saa mbili itawakutanisha nguli wa muziki wa Afrika ambao kutoka katika nchi zao watakutana pamoja mtandaoni kukonga nyoyo za mashabiki wao ambao hawajaonana nao kwa muda sasa.

Tanzania itawakilishwa na wasanii wawili; Diamond Platnumz na Nandy huku Kenya itawatoa Sauti Sol na Bebe Cool itaiwakilisha Uganda. 

Lakini atakuwepo mama “Pata pata” mwenye Grammy (tuzo za kimataifa zinazotambua mchango wa watu kwenye sekta ya muziki) yake siyo mwingine ni Angélique Kidjo wa nchi ya Benin.


Zinazohusiana


Tulia! Bado orodha inaendelea. Kutoka Afrika Magharibi, yupo  Burna Boy, Yemi Alade, Teni, Tiwa Savage, Seun Kuti, Rema na Adekunle Gold hao wote ni kutoka Nigeria.

Kule kwa Madiba, watakaotoa burudani ni rapa AKA na mwana dada aliyesumbua spika za watu kwa kibao cha “John Cena”, Sho Madjozi.

Hakika haiwezi kukamilika bila miuno ya Kikongo kutoka kwa Fally Ipupa au vipi? Na kama haujafahamu bado, atakayesherehesha shoo hii ni muigizaji maarufu mwenye cheo chake. Ni Idriss Elba.

Kufurahia shoo hiyo, siyo haba ukawa na bando la kutosha kutazama mtandao wa YouTube au chaneli ya MTV kwenye king’amuzi. Fuatilia kurasa za WanAfrica kufahamu orodha yote ya wasanii ambao utawatazama.

Tamsha hilo litazidi kudhihirisha umoja walionao Wafrika katika maendeleo ya bara lao.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV