Rais Samia atunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima

June 4, 2026 4:52 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema tuyo hiyo ni ishara ya urafiki kati ya Tanzania na Urusi.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha RUDN nchini Urusi, kwa kutambua mchango wake katika uongozi bora, diplomasia na maendeleo ya jamii.

Rais Samia aliyekuwa akihutubia leo Juni 4, ,2026 katika chuo baada ya kupokea tuzo amesema heshima hiyo ni ishara ya urafiki wa muda mrefu kati ya Tanzania na Urusi pamoja na mchango wa elimu katika kujenga uelewano wa kimataifa.

Ameongeza kuwa RUDN imekuwa daraja muhimu la kuunganisha mataifa na tamaduni mbalimbali duniani kwa kuamini kuwa maarifa yanapaswa kutumika kuleta maendeleo ya binadamu na siyo mgawanyiko.

“Maarifa hayapaswi kuwa chanzo cha mgawanyiko. Yanapaswa kuwa daraja la kuleta uelewano, ushirikiano na maendeleo ya pamoja ya binadamu,” amesema Rais Samia. 

Hii inakuwa shahada ya nane ya heshima kutunukiwa kwa Rais Samia kutoka mataifa mbalimbali, jambo linaloakisi matokeo ya juhudi zake katika kutekeleza mageuzi ya kiuchumi, kuimarisha diplomasia, na kusimamia maendeleo ya kijamii, masuala yanayofanya mchango wake kutambulika zaidi duniani.

Aidha,Rais Samia amekumbusha kuwa zaidi ya Watanzania 5,000 wamewahi kusoma katika vyuo vya Urusi na iliyokuwa Umoja wa Kisovieti, huku wengi wanaorejea nchini humo hutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.

Amesema dunia inakabiliwa na mapinduzi ya teknolojia, ikiwamo akili mnemba, robotiki na sayansi ya data, hivyo kuifanya elimu kuwa nyenzo muhimu ya ushindani wa mataifa. 

“Miundombinu pekee haiwezi kubadilisha taifa. Mabadiliko yanahitaji watu wenye maarifa, ubunifu na uwezo wa kutatua changamoto za wakati wao,” amesema.

Mbali na biashara na elimu, Tanzania na Urusi zimeendelea kudumisha ushirikiano wa muda mrefu katika sekta ya ulinzi na usalama.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV