Daniel Sillo achaguliwa Naibu Spika  Bunge la 13 Tanzania

November 13, 2025 3:22 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Apata asilimia 100 za kura za ndio zilizopigwa na wabunge 371 waliohudhuria kikao.

Dar es Salaam. Wabunge wamechagua Daniel Sillo kuwa Naibu Spika wa Bunge baada ya kumpa kura zote za ndio sawa na asilimia 100 ya kura zilizopigwa na wabunge 371 waliohudhuria kikao

Uchaguzi wa Sillo umefanyika kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, inayobainisha kwamba Naibu Spika atachaguliwa na wabunge kutoka wabunge waliochaguliwa, na kupigiwa kura baada ya kupendekezwa.

Sillo ni Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini ambaye kwa uzoefu pia, amewahi kushika nafasi ya Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.

Wakati Sillo akichaguliwa, Bunge linaendelea kujiandaa kusikiliza hotuba ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambaye anatarajia kulihutubia Bunge hapo kesho Novemba 14, 2025 kama ilivyo kwa mujibu wa sheria. 

Shughuli za Bunge katika kikao cha leo zilikuwa ni kuchagua Naibu Spika wa Bunge pamoja na kumpitisha Waziri Mkuu wa Tanzania ambapo Rais Samia amempendekeza aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba na wabunge kumptitisha kwa kura 369 za ndio akirithi nafasi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Kassim Majaliwa. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV