Rais Samia ateua sita, kuwa wabunge wa Tanzania

November 10, 2025 5:27 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Miongoni mwa walioteuliwa ni pamoja na Dorothy Gwajima na Balozi Mahmoud Thabit Kombo .

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wabunge sita wa Bunge la Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo Novemba 10, 205 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka imeeleza kuwa uteuzi huo ni kwa mujibu wa  Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977.

Miongoni mwa walioteuliwa ni pamoja na Dk Dorothy Gwajima, Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Balozi Dk Bashiru Ally Kakurwa.

Vile vile, amewateua  Abdullah Ali Mwinyi, Balozi Khamis Mussa Omarna na Dk Rhimo Simeon Nyansaho.

Uteuzi huu unakuja siku saba  baada ya Rais Samia kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Kwa mujibu wa Matokeo rasmi yaliyotangazwa Novemba 1, 2025 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ramadhan Kairima, Samia, alitangazwa mshindi baada ya kupata kura milioni 31.91 sawa na asilimia 97.66 ya kura halali milioni 32.67 zilizopigwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks