Sekta ya fedha inavyoimarika Tanzania
- Ukuaji huo umejidhihirisha kupitia ongezeko la idadi ya benki, taasisi za huduma ndogo za fedha, mawakala wa benki pamoja na rasilimali za kibenki.
Dar es Salaam. Katika siku za hivi karibuni, sekta ya fedha nchini Tanzania imeendelea kuonesha mwelekeo chanya wa ukuaji, ikichochewa na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi, upanuzi wa taasisi za kifedha na kuimarika kwa imani ya wananchi katika mifumo rasmi ya fedha.
Ukuaji huo umejidhihirisha kupitia ongezeko la idadi ya benki, taasisi za huduma ndogo za fedha, mawakala wa benki pamoja na rasilimali za kibenki, hali inayoashiria kuimarika kwa mchango wa sekta hiyo katika maendeleo ya uchumi wa taifa.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula aliyekuwa akizungumza Januari 21, 2025 katika uzinduzi maadhimisho ya kitaifa ya wiki ya huduma ya fedha, amesema hadi kufikia Septemba 2025, Tanzania ilikuwa na jumla ya benki za kibiashara 35, benki za kijamii mbili, benki za maendeleo mbili pamoja na benki tatu za huduma ndogo za fedha.
Aidha, taasisi 2,811 za huduma ndogo za fedha pamoja na vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha 70,913 zilisajiliwa, huku taasisi mbili za ubadilishanaji wa fedha zikiongeza idadi ya watoa huduma rasmi nchini.
Aidha, Luswetula ameeleza kuwa upanuzi huo umeenda sambamba na ongezeko kubwa la mawakala wa benki nchini. Ambapo Idadi ya mawakala wa benki imeongezeka kutoka 106,176 hadi kufikia 145,430, jambo linalorahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha hadi ngazi ya jamii.
Mbali na ongezeko la taasisi, rasilimali za kibenki nazo zimeendelea kuimarika na kufikia Sh71.8 trilioni Septemba 2025, ikilinganishwa na Sh62.2 trilioni zilizorekodiwa Septemba 2024.
Aidha, katika kipindi kama hicho, amana za benki zimeongezeka hadi Sh50.2 trilioni kutoka Sh42.7 trilioni mwaka uliotangulia, hatua inayotafsiriwa kama ishara ya kuongezeka kwa imani ya wananchi katika sekta ya fedha.
Katika maelezo yake, Luswetula pia amebainisha kuwa mikopo kwa sekta binafsi imekua kwa kasi kubwa. Ikiongezeka na kufikia Sh42 trilioni mwaka 2025 kutoka Sh35 trilioni mwaka 2024, sawa na ukuaji wa asilimia 24.
Hata hivyo, pamoja na ongezeko la mikopo, amebainisha kiwango cha mikopo chechefu bado kiko katika hali inayodhibitiwa.
“Mikopo chechefu imeongezeka kwa asilimia 2.78, kiwango ambacho bado kipo ndani ya ukomo wa kisheria wa asilimia tano,” ameeleza Luswetula.
Soko la hisa laongezeka
Kwa upande wa sekta ndogo ya mitaji na dhamana, Luswetula amesema Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) limeendelea kukua ambapo kuonesha ukuaji idadi ya kampuni zilizosajiliwa katika soko hilo imefikia 28 huku mifuko ya uwezeshaji ikifikia 21.
Aidha, ameainisha kuwa thamani ya uwekezaji katika masoko ya mitaji ilifikia Sh63.7 trilioni katika kipindi kilichoishia Desemba 2025.
“Jumla ya mauzo ya hisa na hati fungani katika soko la hisa la Dar es Salaam yamefikia Sh6.87 trilioni vilevile thamani ya mifuko ya uwekezaji wa pamoja ilifikia Sh4.35 trilioni katika kipindi hicho,” ameongeza Luswetula.
Fahamu mahitaji ya usingizi kwa watoto wachanga
- Usingizi ni muhimu sana kwa ukuaji wa mwili na akili ya mtoto.

Dar es Salaam. Usingizi ni miongoni mwa mahitaji muhimu kwa binadamu, hususan watoto wachanga katika miaka miwili ya mwanzo ya maisha yao.
Tofauti na watu wazima, watoto huhitaji muda mwingi zaidi wa kulala ili kuwawezesha kukua vizuri na kuimarisha uwezo wa ubongo kufanya kazi kwa ufanisi.
Kwa mujibu wa tovuti ya masuala ya afya ya Stanford Medicine Children’s Health, watoto wachanga huhitaji hadi saa 17 za usingizi kwa siku, ambazo hugawanyika katika vipindi mbalimbali.
“Ratiba ya usingizi wa mtoto ni muhimu sana kwa ukuaji wake wa mwili, maendeleo ya akili (kumbukumbu, kujifunza na umakini), udhibiti wa hisia, pamoja na ujuzi wa mwendo wa mwili,” inaeleza tovuti hiyo.
Tovuti hiyo inabainisha kuwa watoto wenye umri wa kuanzia siku moja hadi miezi mitatu ya mwanzo wanahitaji kulala wastani wa saa 16 hadi 17 kwa siku, lakini mara nyingi hawalali zaidi ya saa 1 hadi 2 kwa wakati mmoja.
Aidha, watoto wenye umri wa miezi minne hadi 12 wanahitaji kulala wastani wa saa 12 hadi 16 kwa siku, huku wale wenye umri wa mwaka mmoja hadi miaka miwili wakihitaji kulala kati ya saa 11 hadi 14 kwa siku.
Tanzania kinara idadi ya Simba Afrika

Shirika la World Population Review limeitaja Tanzania kuwa na simba 14,500 idadi inayoifanya kuwa kinara wa idadi kubwa ya Simba barani Afrika.
Katika mbuga zake za kitaifa na mapori ya akiba nchini Tanzania, unaweza kuona simba jike wakiwinda alfajiri, madume wakinguruma na wengine wakiwinda au kupumzika katika vivuli vya miti.
Unaweza kujionea wanyama hao katika hifadhi mbalimbali ikiwemo Serengeti, Ngorongoro, Tarangire na Ruaha.
Hata hivyo, takwimu hizo zinatofautiana na zile zilizotolewa na IUCN pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ambao waliripoti idadi ya simba hao kuwa 17,000.
Nchi nyingine yenye idadi kubwa ya simba ni Afrika Kusini (Simba 3,284), Botswana (Simba 3,063), Kenya (Simba 2,515) na Zambia (Simba 2,500)
Pamoja na hayo, Tawiri ilibainisha kuwa Tanzania imeongoza barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya wanyama wengine ikiwemo Nyati na Chui.
Fahamu faida za kutumia mifumo rasmi ya fedha

Dar es salaam: Matumizi ya mifumo rasmi ya fedha ni nguzo muhimu katika kuimarisha ustawi wa kifedha wa mtu mmoja mmoja na maendeleo ya uchumi ya Taifa kwa ujumla.
Kupitia mifumo hiyo, ikiwemo benki, taasisi za fedha zilizosajiliwa na huduma za bima wananchi hupata usalama wa fedha zao, uwazi wa miamala na ufuatiliaji sahihi wa mapato na matumizi.
Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mifumo rasmi hupunguza hatari ya wizi, upotevu wa fedha na ulaghai, huku ikirahisisha malipo ya huduma mbalimbali kama ada, kodi na mishahara kwa njia salama na za haraka.
Aidha, akiba inayowekwa kwenye mifumo rasmi inalindwa kisheria, hupata riba, na hujenga historia ya kifedha (credit history) ambayo humwezesha mhusika kupata mikopo kwa ajili ya uwekezaji, biashara au mahitaji ya kijamii.
Kwa ujumla, kutumia mifumo rasmi ya fedha ni msingi muhimu wa ukuaji endelevu wa uchumi, unaochochea uwajibikaji, ufanisi na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Mawaziri Wakuu wa Tanzania tangu uhuru

Dar es Salaam. Tangu Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961, nafasi ya Waziri Mkuu imekuwa mhimili muhimu katika uendeshaji wa serikali na utekelezaji wa sera za taifa. Kuanzia kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika, hadi kwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa sasa.
Tanzania imepitia viongozi waliotoa mchango mkubwa katika kuimarisha utawala, uchumi, na amani ya nchi. Wengine waliowahi kushika nafasi hiyo ni pamoja na Rashidi Kawawa, Edward Sokoine, Cleopa Msuya, Salim Ahmed Salim, Joseph Warioba, John Malecela, Frederick Sumaye, Edward Lowassa, na Mizengo Pinda.
Kila mmoja ameacha alama katika historia ya uongozi wa taifa, lakini je, ni nani atakwenda kurithi nafasi hiyo kutoka kwa Waziri Mkuu wa sasa Kassim Majaliwa ?
Maspika wa Bunge la Tanzania tangu uhuru
Dar es Salaam. Tangu kupatikana kwa uhuru mwaka 1961, Tanzania imepata viongozi kadhaa waliowahi kushika nafasi ya Spika wa Bunge. Spika wa kwanza alikuwa A.Y.A. Karimjee, aliyeliongoza Bunge la Tanganyika kuanzia mwaka 1956 hadi 1962.
Baada ya hapo, nafasi hiyo ilishikiliwa na Chief Adam Sapi Mkwawa, ambaye alihudumu kwa kipindi kirefu zaidi kuanzia mwaka 1962 hadi 1973, na tena kati ya mwaka 1975 hadi 1994.
Chief Erasto Mang’enya aliongoza kwa muda mfupi kati ya mwaka 1973 na 1975, kabla ya Pius Msekwa kuchukua nafasi hiyo mwaka 1994 na kuhudumu hadi 2005.

Wengine waliowahi kushika nafasi hiyo ni Samuel Sitta (2005–2010), Anne Makinda (2010–2015), Job Ndugai (2015–2022), na kwa sasa Dk. Tulia Ackson, ambaye alianza Februari 2022 na ambaye ukomo wake unakwenda kufikia Novemba 11, 2025 atakapa chaguliwa Spika mpya.
Kwa zaidi ya nusu karne, Bunge limepitia mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiutendaji chini ya uongozi wa maspika hao. Hata hivyo, swali linaloibuka sasa ni, nani atarithi mikoba ya Dk. Tulia Ackson na kuwa Spika wa Bunge la 13 la Tanzania?
Foundation targets school facilities to strengthen education in Tanzania
- The Sanjeev Mansotra Foundation (SMF) will support the renovation and expansion of four schools in Dodoma.
- These changes aim to make schools safer, cleaner, and more exciting places to learn.
Dar es Salaam. Students in Dodoma city are expected to see better classrooms, more learning materials, and improved school facilities following the launch of the Sanjeev Mansotra Foundation (SMF) in Tanzania.
The Foundation, started by Sanjeev Mansotra, Chairman of Planet One Group, will first support the renovation and expansion of four schools in the city.
The work will include building new classrooms, science laboratories, and libraries. It will also provide school uniforms, stationery, clean drinking water, and health camps for students and nearby communities.
These changes aim to make schools safer, cleaner, and more exciting places to learn.
“The establishment of this foundation is rooted in my firm belief that education is the cornerstone of a thriving national economy,” said Mansotra. “By expanding access to quality education, we empower individuals and lay the foundation for sustainable economic growth and prosperity.”
The Foundation’s launch comes at a time when many African children still struggle to access education.
A joint report by United Nations Education, Science and Culture Organization (UNESCO), United Nations International Children’s Emergency Fund (UNICEF), and the African Union shows that while school enrollment has grown by 75 million since 2015, more than 100 million children remain out of school.
The same report says four out of five African children aged 10 cannot read and understand a simple story.

Investing in children education is crucial part of building literate community that lead to better life. Photo | Idea For Good.
In Tanzania, and especially in rural areas, many students face challenges such as long distances to school, lack of classrooms, and poor sanitation. These problems lower attendance and performance. SMF hopes to close this gap by supporting both students and teachers.
“By investing in infrastructure and essential resources, we aim to inspire students and teachers alike, boost enrollment, and improve learning outcomes,” Mansotra said at the launch of SMF in Dodoma on November 5, 2025.
The Dodoma City Council, which manages public schools in the region, invited the foundation to support local education projects. Local leaders have welcomed the plan, saying it will help hundreds of children and ease the pressure on crowded schools.
The Foundation plans to expand its projects to Ghana, Guinea, Togo, Sierra Leone, and India in the future. It will continue to focus on education, health, and improving the lives of underserved communities.
“Our long-term vision is to serve as a catalyst for transformative change. We are deeply committed to nurturing the next generation by equipping them with education, skills, and aptitude they need to thrive. From imagination to impact, our mission is to ensure no one is left behind,” Mansotra concluded.
For Dodoma’s young learners, this initiative offers more than just buildings, it brings hope for a better future, where every child has the chance to learn and succeed.



