BoT yatangaza mnada wa hadhara, fursa kwa Watanzania kununua vifaa kwa bei nafuu

February 6, 2026 5:01 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Vifaa vitakavyouzwa ni pamoja na magari, pikipiki, mitambo, vifaa vya ofisini, vifaa vya tehama na vifaa vingine.
  • Ni fursa kwa Watanzania wenye uhitaji kupata vifaa vya thamani kwa bei nafuu.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kufanya mnada wa hadhara kuuza vifaa chakavu ikiwemo magari, pikipiki, mitambo, vifaa vya ofisini, vifaa vya tehama na vifaa vingine katika ofisi zilizopo maeneo mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BoT mnada huo unatarajiwa kufanyika tarehe tofauti kuanzia Februari 18 mpaka Februari 28, 2026 katika ofisi za BoT zilizopo mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Mtwara na Mjini Magharibi.

Taarifa hiyo inabainisha kuwa mali zitakazouzwa zitauzwa katika uchakavu wake kutokea mahali zilipo. 

Masharti ya mnada

Kwa mujibu wa BoT, malipo ya vifaa chakavu ni asilimia 100 na mteja atatakiwa kuondosha vifaa alivyonunua siku ya mnada.

Kwa mnunuzi wa gari, pikipiki na mitambo atatakiwa kulipia papo hapo amana “deposit” isiyopungua asilimia 25 ya bei ya kifaa atakachonunua na kukamilisha malipo yote ndani ya muda wa siku 14 kuanzia tarehe ya mnada.

“Mnunuzi akishindwa kutimiza sharti hilo atakosa haki zote za ununuzi na amana iliyolipwa haitarudishwa,” imesisitiza taarifa hiyo.

Aidha, mnunuzi atatakiwa kuondoa au kuchukua mali hiyo aliyonunua ndani ya muda wa siku saba kuanzia siku ya kukamilisha malipo huku ubadilsihaji wa umiliki ukibaki juu yake.

Kutangazwa kwa mnada huo ni fursa muhimu kwa Watanzania wenye mtaji mdogo na ambao wana uhitaji wa vifaa kwa ajili ya kuanzisha biashara au matumizi binafsi kwani wataweza kupata vifaa vya thamani kwa bei nafuu. 

Bot imeelekeza kuwa ruhusa ya kuangalia vifaa itatolewa siku mbili kabla ya mnada husika kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Katika siku zote za zoezi la mnada utaanza saa nne asubuhi katika vituo vilivyoorodheshwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks