Biashara, watu binafsi wanavyonufaika mikopo sekta binafsi Tanzania

March 30, 2020 9:19 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Sehemu kubwa ya mikopo kwa sekta binafsi imeelekezwa kwa watu binafsi au kaya ambazo zilipata wastani wa asilimia 29.6 ya mikopo yote na shughuli za biashara (asilimia 17.9).
  • Mikopo kwa sekta binafsi imeongezeka kwa wastani wa asilimia 9.1 katika mwaka ulioishia Januari 2020 ikilinganishwa na asilimia 7.3 iliyorekidiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2019.

Dar es Salaam. Wakati mikopo inayoelekezwa kwa sekta binafsi ikiongezeka kwa asilimia 9.1 ndani ya mwaka mmoja uliopita, sehemu kubwa ya mikopo hiyo imekuwa ikiwanufaisha zaidi watu binafsi ambao wanamiliki shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo biashara.

Ripoti ya Tathmini ya Uchumi ya mwezi Februari 2020 (Economic Monthly Review) iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) hivi karibuni inaeleza kuwa mikopo kwa sekta binafsi imeongezeka kwa wastani wa asilimia 9.1 katika mwaka ulioishia Januari 2020 ikilinganishwa na asilimia 7.3 iliyorekidiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2019.

“Kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa mikopo hiyo kulichangiwa na usimamizi thabiti wa sera ya fedha, ongezeko la shughuli za kiuchumi na jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali za kuboresha mazingira ya biashara,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo inayopatikana pia katika tovuti ya BoT.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa sehemu kubwa ya mikopo kwa sekta binafsi imeendelea kuelekezwa kwa watu binafsi au kaya ambazo zilipata wastani wa asilimia 29.6 ya mikopo yote ikifuatiwa na shughuli za biashara zilizokuwa na wastani wa asilimia 17.9.

Sekta nyingine zilizonufaika na mikopo hiyo ni pamoja na ujenzi, kilimo, usafirishaji na mawasiliano, madini, hoteli na migahawa.  


Soma zaidi:


Mikopo inayoelekezwa katika shughuli zote kubwa za uchumi imeendelea kuongezeka, isipokuwa kwa shughuli za hoteli na migahawa ambayo ilishuka kwa asilimia 10.3 katika kipindi hicho. 

Hata wakati mikopo kwa sekta binafsi ikiongezeka, riba zinazotozwa na benki za biashara nayo imeshuka, jambo ambalo ni kiasharia kizuri kwa ukuaji wa sekta ya fedha na uchumi,

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, riba iliyotozwa kwenye mikopo iliyotolewa na benki ilikuwa wastani wa asilimia 16.7 mwezi Januari 2020 ikishuka kutoka wastani wa asilimia 17.3 katika kipindi kama hicho 2018.

Benki kutoza riba ndogo, kunatoa fursa kwa wananchi wengi zaidi wakiwemo wakulima na wafanyabiashara kunufaika na mikopo inayotolewa na taasisi hizo za fedha kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV