Benki ya Dunia: Uchumi wa Tanzania kukua hadi asilimia 5.3 mwaka 2021

March 3, 2021 1:19 pm · Nuzulack Dausen
Share
Tweet
Copy Link
  • Imesema utakua kwa kasi ya kati ya wastani wa asilimia 3 hadi asilimia 5.3 mwaka 2021.
  • Hiyo inatokana na kuanza kuimarika kwa shughuli za kiuchumi duniani kutokana na uwepo wa jitihada za kutoa chanjo ya ugonjwa wa virusi vya corona.

Dar es Salaam. Benki ya Dunia (WB) imesema inatarajia kuwa uchumi wa Tanzania utakua kwa kasi ya kati ya wastani wa asilimia 3 hadi asilimia 5.3 mwaka 2021 ukichangiwa zaidi na kuanza kuimarika kwa shughuli za kiuchumi duniani kutokana na uwepo wa jitihada za kutoa chanjo ya ugonjwa wa virusi vya corona.

Kiwango hicho cha ukuaji wa uchumi kinachotarajiwa na Benki ya Dunia ni chini ya matarajio ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inayotarajia kuwa uchumi utakuwa kwa asilimia 6 au zaidi mwaka 2021.

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe, Mara Warwick ameeleza leo katika uzinduzi wa ripoti mpya ya uchumi kuwa Tanzania ilifanya vema mwaka 2020 ikilinganishwa na nchi nyingine katika ukanda wake lakini kasi ya ukuaji uchumi ilishuka na umaskini unatarajiwa kuongezeka kutokana na changamoto za kiuchumi zinazotokana na athari za corona.

 “Kasi ya ukuaji wa uchumi ilishuka kutoka asilimia 5.8 mwaka 2019 hadi kufikia kiwango kinachokadiriwa kuwa asilimia 2 mwaka 2020 na wastani wa ukuaji wa pato la mtu ulishuka hadi ukuaji hasi kwa mara ya kwanza ndani ya zaidi ya miaka 25,” amesema Warwick.


Zinazohusiana:


Hata hivyo, kiwango cha ukuaji wa ukuaji wa uchumi mwaka 2020 cha Benki ya Dunia kinatofautiana na  BoT ya kuwa matarajio ya ukuaji wa uchumi wa asilimia 5.5 yatafikiwa kama ilivyotarajiwa na Serikali kutokana na jitihada madhubuti ya kudhibiti athari za ugonjwa wa corona kwenye uchumi.

Katika mwaka 2021, Warwick anasema benki hiyo inatarajia kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi itakuwa kati ya asilimia 3 hadi asilimia 5.3 huku matokeo makubwa zaidi ya hayo yakitazamiwa zaidi katika kuimarika kwa shughuli za kiuchumi zinazochagizwa na jitihada za kusambaza chanjo za kukabiliana na corona na utendaji imara wa kuimarisha uchumi huo.

Warwick ameeleza kuwa tofauti na nchi nyingine zilizopo ndani ya kanda moja, Tanzania bado ina fursa ya kuweza kuimarisha uchumi wake haraka kutokana na uwepo wa viashiria imara vya kiuchumi ikiwemo deni himilivu. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV