Idadi ya watalii Tanzania yaongezeka kwa asilimia 25.7

Lucy Samson 0423Hrs   Oktoba 11, 2023 Safari
  • Ongezeko hilo linafanya kuwa na jumla ya watalii 1,131,286 waliotembelea Tanzania.
  • Asilimia 3.3 kati yao waliingia nchini kupitia visiwani Zanzibar.

Dar es Salaam.Idadi ya watalii walioingia Tanzania imeongezeka kwa asilimia 25.7 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja huku nchi za Amerika na Ufaransa zikiingiza idadi kubwa zaidi ya watalii.

Kwa mujibu wa takwimu zinazotolewa na za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) hadi kufikia Agosti 2023 watalii 1,131,286  waliingia nchini ulinganisha na watalii 900,182  waliorekodiwa Agosti mwaka jana.

NBS inafafanua kuwa asilimia 3.3 ya watalii hao waliingia nchini kupitia visiwani Zanzibar kunakosifika kwa vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo misitu ya viungo vya kupikia na  maeneo ya kihistoria.

“Kati ya watali wote walioingia nchini, watalii 336,203 waliingia kupitia Zanzibar, sawa na asilimia 31.1 ya watalii wote,” imesema taarifa ya NBS.

Miongoni mwa mataifa yalioongoza kwa kuingiza watalii wengi kutoka nje ya bara la Afrika ni pamoja na Marekani  watalii 84,541, Ufaransa (72,009), Ujerumani (57,798), Uingereza (51,505) na Italia  watalii 51,056.

Watalii kutoka ndani ya bara la Afrika ni pamoja na Kenya watalii 128,753, Burundi (69,505), Zambia (38,394), Rwanda (37,269) na Uganda watalii 28,594

Related Post