Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi yapaa kwa zaidi ya asilimia 300

May 15, 2024 4:50 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Waziri Abdallah Ulega aomba Bunge lipitishe Sh 460.3 bilioni kwa ajili ya matumizi ya wizara kwa mwaka 2024/25.
  • Utolewaji wa fedha za maendeleo bado unasua sua.

Dar es Salaam. Huenda sekta ya uvuvi na ufugaji ikapata msukumo mpya baada ya Serikali kuongeza bajeti kwa asilimia 310 katika mwaka 2024/25 ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kurekodiwa kulinganisha na miaka iliyopita.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega aliyekuwa akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha utakaoanza Julai, 2024 bungeni Dodoma leo Mei 14, 2024 ameliomba bunge kuidhinisha kiasi cha Sh 460.3 bilioni kwa ajili ya matumizi ya wizara hiyo.

“Kati ya fedha hizo, Sh 97.2 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh 363.1 bilioni  ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo,” amesema Ulega.

Bajeti hiyo kwa mwaka 2024/25 imeongezeka kwa Sh 348.2 bilioni ikiwa ni mara 310 zaidi ya Sh 112.3 bilioni iliyoidhinishwa kwa mwaka 2023/2024 unaoishia Juni 30 mwaka huu.

Hadi Aprili, 2024, jumla ya Sh 44.5 bilioni zimetolewa, ikiwa ni sawa na asilimia 39 ya bajeti nzima ya wizara hiyo.


Soma zaidi:Bajeti ya Wizara ya Afya yaongezeka kwa asilimia 6


Utolewaji wa fedha za maendeleo bado bado

Licha ya bajeti ya wizara hiyo na fedha za maendeleo kuongezeka mwaka hadi mwaka mwaka bado fedha hizo hazitolewi kwa wakati jambo linaloathiri utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kwa mwaka 2023/24 wizara iliidhinishiwa Sh 61.9 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo  sawa na asilimia 55 ya bajeti nzima ya wizara kwa mwaka huo.

Hadi kufikia Aprili 2024 ni asilimia 20.1 tu ya bajeti ya maendeleo imetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya wizara hiyo.

Ufinyu huo wa fedha za maendeleo umeibuka pia katika ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo iliyowasilishwa na Ng’wasi Kamani Mbunge wa viti maalum (CCM).

Kamani amesema kuwa mwenendo hafifu wa utolewaji wa fedha hizo utazifanya sekta hizo kutokamilisha miradi yake kwa wakati jambo litakaloathiri uchumi wa Taifa na mwananchi mmoja mmoja.

“Hali hii siyo nzuri inaweza kusababisha sekta ya mifugo kushindwa kuchangia vyema katika pato la taifa, kukuza ajira na kupunguza umaskini miongoni mwa watanzania waliojiajiri katika sekta hii,” amesema Ng’wasi.

Aida, Ulega amewaambia wabunge kuwa kwa mwaka 2024/25 wizara yake itatekeleza vipaumbele mbalimbali ikiwemo kukamilisha ujenzi wa mabwawa saba, visima virefu vitatu, kukamilisha ujenzi wa bandari ya uvuvi Kilwa – Masoko na kufanya maandalizi ya awali ya ujenzi wa bandari ya uvuvi ya Bagamoyo.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV