Ahueni bei ya petroli, dizeli mafuta ya taa ikishuka

July 1, 2026 7:13 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya rejareja ya petroli kuuzwa Sh3,990,  dizeli Sh4,182 na mafuta ya taa kwa Sh4,443.

Arusha. Huenda watumiaji wa vyombo vya moto nchini Tanzania wakashuhudia ahueni kiduchu mara baada ya bei ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa mwezi Julai kushuka kulinganisha na ile iliyokuwa ikitumika mwezi Juni.

Taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Julai Mosi, 2026 inabainisha kuwa bei hizo zimepungua kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

“Hivyo, kutokana na kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia, bei za mafuta katika soko la hapa nchini zinashuka kwa Shilingi 96 kwa lita ya petroli, Shilingi 151 kwa lita ya dizeli na Shilingi 242 kwa lita ya mafuta ya taa,” imesema taarifa ya Ewura.

Kushuka kwa bei hizo kutaifanya bei ya rejareja ya mafuta yanayopitia Bandari ya Dar es Salaam kuuzwa Sh3,990 kwa lita moja ya petroli, dizeli Sh4,182 na mafuta ya taa kwa Sh4,443.

Bei hizo zimeshuka kutoka Sh4,086 iliyotumika kununua lita moja ya petroli mwezi Juni na Sh4,333 dizeli.

Ahueni hiyo pia imewafikia watumiaji wa mafuta yanayopitia bandari nyingine ikiwemo Bandari ya Tanga ambapo lita moja ya petroli inanunuliwa kwa Sh4,051, petroli kwa Sh4,243 na mafuta ya taa kwa Sh4,504.

Kwa upande wa mafuta yanayotokea Bandari ya Mtwara katika mwezi Julai yatauzwa kwa Sh4,083 kwa petroli, Sh4,275 dizeli na Sh4,536 kwa lita moja ya mafuta ya taa.

Ahueni kiduchu baada ya maumivu ya miezi minne

Watumiaji wa vyombo vya moto nchini Tanzania wanashuhudia ahueni ya bei ya mafuta kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita ya Irani, Marekani pamoja na Israeli iliyosababisha uharibifu wa miundombinu ya uzalishaji na usafirishaji wa mafuta pammoja na  kupunguza upatikanaji wa bidhaa hiyo duniani,

Kabla ya vita hiyo kuanza mwishoni mwa wezi Februari lita moja ya petroli ilikuwa inauzwa Sh2,788, dizeli iliuzwa kwa Sh2,701 suala lililotoa ahueni kwa watumiaji hao wa vyombo vya moto.

Kwa bei hizo mpya za mwezi Julai, Sh10,000 itatumika kununua lita 2.5 za petroli kulinganisha na lita 2.4 zilizopatikana mwezi uliopita huku watumiaji wa dizeli wakipata lita 2.39 kutoka lita  2.3 zilizokuwa zikipatiikana awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
2 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
2 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Msikie Jaji Mkuu Masaju : Mambo wasiopaswa kufanya madalali wa Mahakama.

Msikie Jaji Mkuu Masaju : Mambo wasiopaswa kufanya madalali wa Mahakama.

Nukta TV

Dk Mwigulu: Kama siyo Rais Magufuli mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere usingefanyika

Dk Mwigulu: Kama siyo Rais Magufuli mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere usingefanyika

Nukta TV

Umuhimu wa elimu ya mikopo

Umuhimu wa elimu ya mikopo

Nukta TV