TBL yatangaza gawio la Sh529 kwa hisa 2025

April 27, 2026 4:27 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Gawio hilo limepungua kwa asilimia 35.3 kutoka Sh818 kwa kila hisa la mwaka 2024.

Dar es Salaam. Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imetangaza kutoa gawio la awali la Sh529 kwa kila hisa kwa mwaka ulioishia Desemba 31, 2025, kiwango kilichoshuka kwa Sh289 kutoka gawio lililotangazwa mwaka 2024.

Kwa mujibu wa taarifa ya TBL, bodi ya wakurugenzi imeidhinisha malipo hayo yanayotarajiwa kuanza kutolewa kufikia Mei 27, 2026, yakilipwa moja kwa moja kwenye akaunti za benki au mifumo ya fedha za simu za wanahisa.

Gawio hilo lililotangazwa na TBL limeshuka kwa asilimia 35 ikilinganishwa na gawio la awali la Sh818 kwa kila hisa lililotangazwa kwa mwaka ulioishia Desemba 31, 2024.

Hii ina maanisha kuwa kiasi cha mapato kwa wahisa waliowekeza kwenye kampuni hiyo kinakwenda kupungua kulinganisha kiasi walichukipata katika mwaka unaoishia Desemba 2024.

Kwa kawaida, gawio hushuka hutokana na kupungua kwa faida ya kampuni baada ya kodi jambo ambalo hulazimisha bodi kupunguza kiwango cha fedha ambacho hutolewa kwa wanahisa kama faida ya uwekezaji wao. 

Hata hivyo, hadi wakati soko la DSE linafungwa Aprili 27, 2026 bei ya hisa moja ya TBL ilifikia Sh10,000 ikiwa ni ongezeko la Sh120 kwa kila hisa kutoka bei iliyorekodiwa Aprili 24, 2026 ya Sh9,880, hatua iliyofanya wawekezaji walale na tabasamu. 

Licha ya gawio kushuka bado TBL ni moja ya kampuni zilizotoa kiwango kikubwa cha gawio kwa hisa kwa mwaka wa fedha wa 2025. Pia, hisa za kampuni hiyo ni miongoni mwa hisa ghali zaidi DSE. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI, WIZARA YA MADINI IKIWASILISHWA BUNGENI

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI, WIZARA YA MADINI IKIWASILISHWA BUNGENI

Nukta TV

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Nukta Africa kuzindua Nukta AI, siku ya uhuru wa vyombo vya habari

Nukta Africa kuzindua Nukta AI, siku ya uhuru wa vyombo vya habari

Nukta TV