Wanahisa NMB wagawana Sh305.08 bilioni za faida

June 10, 2026 5:27 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Gawio la faida la NMB kwa hisa limeongezeka kwa asilimia 217.8% ndani ya miaka mitano tangu lilipokuwa Sh193 mwaka 2021.

Dar es Salaam. Wahahisa wa NMB wamegawana keki ya Sh305.08 bilioni kama faida ya uwekezaji wao baada ya wanahisa kupitisha pendekezo la Sh610.15 kwa kila hisa kwa mwaka 2025 sawa na ongezeko la Sh181.3 kutoka gawio lililotolewa mwaka 2024.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna amewaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wanahisa 2026 kuwa kiwango hicho ni pendekezo la Bodi ya Wakurugenzi ya NMB iliyopendekeza gawio la kawaida la Sh504.26 pamoja na gawio maalum la Sh105.89 kwa kila hisa. 

Zaipuna amewahakikishia wawekezaji kuwa utolewaji wa gawio hilo hautadhoofisha uwezo wa kifedha wa benki hiyo, akieleza kuwa NMB itaendelea kuwa imara katika utekelezaji wa mikakati yake ikiendelea kuleta thamani kwa wanahisa wake katika miaka ijayo.

“Nataka kuwahakiishia tunao mtaji wa kutosha, mtaji wetu kabla ya kulipa gawio mtaji wetu upo asilimia 24.7, lakini hata baada ya kulipa gawio tutakuwa na asilimia 22.4, kwa hiyo itatuwezesha kufanya biashara na hata tukisema tunakwenda kuwekeza nje bado tutakuwa tunaweza kufanya uwekezaji bila wasiwasi wowote,” amesema Zaipuna 

Ongezeko hilo la gawio lililopitishwa kwa shangwe na kura za kishindo na wahahisa ni sawa na ongezeko la asilimia 42.2 kutoka gawio la Sh428.85 kwa kila hisa la mwaka 2024.

Hii si mara ya kwanza kwa benki hiyo iliyokuwa kwa kasi ndani ya miaka kumi kurekodi ongezeko la gawio kwa kila hisa. Ndani ya miaka mitano gawio limeongezeka kwa asilimia 217.8 tangu lilipokuwa Sh193 mwaka 2021.

Hii inamaanisha kuwa wanahisa waliowekeza katika benki hiyo wanaendelea kutunisha mifuko mwaka hadi mwaka na kula matunda yatokanayo na uwekezaji wao katika benki hiyo iliyoweka rekodi ya kihistoria ya faida ya Sh1.1 trilioni kabla ya kodi mwaka 2025.

Wanahisa washerekea matunda ya uwekezaji wao

Bernard Mhilo, mmoja wa wanahisa waliohudhuria mkutano huo, amesema ongezeko la gawio linaonyesha namna NMB ilivyoendelea kutoa thamani kwa wawekezaji wake, akieleza kuwa uwekezaji huo umekuwa msaada mkubwa katika maisha ya familia yake tangu mama yake, ambaye sasa amestaafu, alipoanza kununua hisa za benki hiyo mwaka 2018.

“Mtu kama mama ambaye sasa amestaafu, gawio hili ni chanzo muhimu cha kipato kinachomsaidia kukidhi mahitaji yake ya kila siku bila kutegemea mshahara ambao kwa sasa hana,” amesema Mhilo.

Kwa sasa, hisa ya NMB ndiyo hisa ghali zaidi katika kampuni zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ambapo mpaka kufikia leo Juni 10, 2026, hisa moja ya NMB inauzwa Sh14,930.

Wahahisa wa NMB wamesema wanaendelea kufurahia kuona uwekezaji wao unazaa matunda mwaka hadi mwaka katika benki hiyo ambayo gawio la faida kwa kila hisa limekuwa kwa zaidi ya asilimia 200. Picha | NMB

Kwa mwekezaji kama Mhilo uwekezaji wake umekuwa kwa asilimia 538 kulinganisha kulinganisha na mwaka 2020 ambapo hisa moja ya NMB ilikuwa Sh2,340.

Itakumbukwa kuwa kiasi cha gawio kilichopitishwa ni kinatokana na kiasi cha Sh305.08 bilioni kilichotengwa kama gawio la faida kutoka katika faida baada ya kodi cha Sh756 bilioni iliyopatikana mwaka 2025. 

Na kwa mujibu wa NMB gawio hilo litagawiwa kwa wahahisa kufikia kuanzia Juni 24, 2026.

Hata hivyo, mbali na kupitisha gawio la Sh610.15 ambalo ni asilimia 43 ya faida, wanahisa pia wamepitisha gawio la asilimia 5 ya faida kwa Wakurugenzi wa benki hiyo kubwa ya kibiashara nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Sin

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Sin

Nukta TV

Mizinga ya heshima, Rais Samia akimpokea Rais wa Singapore, Ikulu Dar es Salaam

Mizinga ya heshima, Rais Samia akimpokea Rais wa Singapore, Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Nukta TV