DSE yaongeza ukomo mabadiliko ya bei hisa za CRDB hadi 10%

April 15, 2026 6:01 pm · Nuzulack Dausen
Share
Tweet
Copy Link
  • Uongozi wa DSE umeongeza mara mbili wigo wa ukomo wa mabadiliko ya bei kwa hisa kwa siku kutoka asilimia 5 hadi 10 ndani ya siku tano za kazi.

Dar es Salaam. Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) limeongeza kwa muda ukomo wa mabadiliko ya bei ya hisa za benki ya biashara ya CRDB kutoka asilimia tano hadi asilimia 10 kwa siku baada ya benki hiyo kutangaza gawio kwa wawekezaji wake. 

CRDB (CRDB Bank PLC) imetangaza leo gawio la Sh90 kwa hisa kwa mwaka wa fedha 2025 baada ya kuripoti faida baada ya kodi ya Sh724.6 bilioni, ikiwa ni kiwango cha juu kurekodiwa tangu kuanzishwa kwa benki hiyo miaka 30 iliyopita. 

Gawio hilo, lililopendekezwa na Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB, ni ongezeko la asilimia 38 ndani ya mwaka mmoja kutoka gawio la Sh65 kwa hisa lilitolewa mwaka 2024, jambo litakalowaacha wawekezaji hao na tabasamu. 

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo Aprili 15, 2026, uongozi wa DSE umesema kuwa ongezeko hilo la ukomo wa mabadiliko ya bei ya hisa litakuwa kwa siku tano za kazi kuanzia leo Aprili 15 hadi 21, 2026. 

Kwa mujibu wa kanuni za DSE, bei ya hisa kwenye soko hilo hairuhusiwi kupanda au kushuka kwa zaidi ya asilimia tano kwa siku moja ya biashara. 

“Soko linahifadhi haki kuchukua hatua nyingine zozote zitakazoonekana zinafaa kuhakikisha kuwa soko linaendeshwa kwa utulivu na utaratibu mzuri unadumishwa,” imesema taarifa ya DSE.

Mara nyingi kampuni iliyoorodheshwa kwenye soko la hisa ikitangaza gawio huwa kuna presha baina ya wawekezaji ya kutaka kununua na kuuza hisa kutokana na kiwango cha gawio husika. 

Katibu wa kampuni wa CRDB Pascal Mihayo amewataka wawekezaji kuwasilisha na kusasisha taarifa zao za malipo katika matawi yaliyo karibu, tovuti ya Benki, App ya CRDB Investor na makao makuu ya CRDB Bank.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
14 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
14 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
14 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV