TRC: Hitilafu ya kiuendeshaji chanzo ajali ya SGR

October 23, 2025 11:30 am · Esau Ng'umbi
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema uchunguzi wa kina na juhudi za kuhakikisha kwamba huduma zinarejea haraka zinaendelea 

Dar es Salaam. Shirika la Reli nchini  (TRC) limesema hitilafu ya kiuendeshaji ndoo chanzo cha ajali ya treni ya umeme iliyokua ikisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma majira ya saa 2:00 asubuhi leo Oktoba 23, 2025 .

Ajali hiyo  imetokea kituo cha Ruvu na kwa taarifa za awali hakuna tukio la kifo.

Taarifa ya TRC iliyotolewa na Mkurugeni Mkuu Mhandisi Machibya Shiwa, imeeleza kuwa kwa sasa timu ya wataalamu ikiongozwa na Katibu Mkuu Uchukuzi,  vyombo vya ulinzi na usalama na menejimenti ya TRC inaendelea na uchunguzi wa kina na juhudi za kuhakikisha kwamba huduma zetu zinarejea haraka

Aidha, TRC imeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa abiria kutokana na ajali hiyo.

Hii ni ajali ya kwanza iliyohusisha mabehewa matatu kuhama nje ya reli, awali zilikuwa zikiripotiwa hitilafu zinazodaiwa kuwa za umeme ambapo safari zilikuwa zikisimama kupisha matengenezo na kisha safari kuendelea.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV