SAUT yasitisha udahili kozi tano mwaka wa masomo 2025/26

July 22, 2025 3:27 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Kozi hizo ni pamoja na Sheria, Sosholojia pamoja na Mahusiano kwa Umma.

Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kimesitisha udahili wa kozi tano za shahada ya kwanza katika mwaka wa masomo 2025/26 ikiwemo za sosholojia (sociology) pamoja na falsafa.

Uamuzi huo umewekwa wazi siku chache tu tangu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kusitisha udahili wa wanafunzi katika programu tisa za shahada ya kwanza za ualimu kwa mwaka wa masomo 2025/2026.

Afisa habari wa chuo cha SAUT Living Komu ameiambia Nukta Habari kuwa uamuzi huo umefikiwa mara baada ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) nchini kutoridhisha na uwiano kati ya walimu na wanafunzi wa kozi hio.

“Ambacho kimesababisha programu hizi zisidahili ni uwiano kati ya wanafunzi na walimu kwenye baadhi ya kozi, uwiano wa TCU nchini lazima uwe sawa yaani kwamba mwalimu mmoja afundishe wanafunzi 50,” ameeleza Komu.

Komu ameeleza kuwa kati ya kozi 14 zinazotolewa chuoni hapo, zilizozuiliwa ni pamoja Shahada ya kwanza ya Sheria, Shahada ya Sanaa katika Sosholojia, Shahada ya Falsafa Pamoja na Elimu, Shahada ya Utalii Usimamizi wa Huduma za Wageni pamoja na Shahada ya Mahusiano kwa Umma.

Hata hivyo, Komu amebainisha kuwa zuio la TCU huwa linatolewa katika muda husika wa masomo na iwapo chuo kikitimiza vigezo basi kozi hurejeshwa tena.

/
No matches found for this filter
27 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
27 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

Nukta TV

MGOMO WA DALDALA WASITISHWA ARUSHA, MADEREVA WAFUNGUKA MAZITO

MGOMO WA DALDALA WASITISHWA ARUSHA, MADEREVA WAFUNGUKA MAZITO

Nukta TV

🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

Nukta TV