Ukatili mtandaoni wapungua 55%, wanaume hatarini  zaidi

October 22, 2026 4:47 pm · Method Allen
Share
Tweet
Copy Link
  • Kati ya matukio yote 213 yaliyorekodiwa, wanaume walikuwa wahanga katika matukio 161, sawa na asilimia 75.6, huku wanawake wakiwa wahanga katika matukio 52, sawa na asilimia 24.4.

Dar es Salaam. Mitandao imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya waliowengi ikiwawezesha kuwasiliana, kufanya biashara au kuifurahisha.

Pamoja na manufaa hayo, matumizi ya mitandao pia yamekuwa yakihusishwa na changamoto mbalimbali za usalama na ustawi wa watumiaji, ikiwemo ukatili mtandaoni (cyberbullying) unaoathiri makundi mbalimbali ya watumiaji.

Ripoti ya Hali ya Uhalifu na Matukio ya Usalama Barabarani inayotolewa na Jeshi la Polisi Tanzania inabainisha kuwa mwaka 2025 kulikuwa na matukio 213 ya ukatili mtandaoni.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, matukio hayo yayohusisha vitendo kama vile kutoa taarifa za uongo, lugha ya matusi, udanganyifu unahusiana na komputa na ubaguzi yalipungua kwa asilimia 55.2 kulinganisha na matukio 453 yaliyoripotiwa mwaka 2024.

Hata hivyo, mbali na kupungua kwa matukio takwimu zikionyesha kuwa wanaume ndio wanaongoza kwa kuwa wahanga wakubwa wa vitendo hivyo ikilinganishwa na wanawake.

Kati ya matukio yote 213 yaliyorekodiwa, wanaume walikuwa wahanga katika matukio 161, sawa na asilimia 75.6, huku wanawake wakiwa wahanga katika matukio 52, sawa na asilimia 24.4.

Elimu sababu matukio kushuka

Pamoja na hatua thabiti zinazochukuliwa na vyombo vya usalama dhidi ya watu wanaokiuka sheria ya makosa ya mtandaoni, ripoti hiyo inabainisha kuwa moja ya sababu zilizochangia kushuka kwa matukio hayo ni ongezeko la kampeni za elimu kuhusu matumizi salama ya mitandao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
22 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
22 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
22 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Uhaba wa maji unavyozitesa jamii za asili, wakiwemo Wahadzabe, Karatu, Tanzania

Uhaba wa maji unavyozitesa jamii za asili, wakiwemo Wahadzabe, Karatu, Tanzania

Nukta TV

Mambo ya kuzingatia unapoanzisha chombo cha habari mtandaoni (ONLINE MEDIA)

Mambo ya kuzingatia unapoanzisha chombo cha habari mtandaoni (ONLINE MEDIA)

Nukta TV

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

Nukta TV