Idadi ya watalii wa kigeni yapaa Tanzania

March 6, 2025 4:12 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link

Tanzania imeendelea kung’ara katika sekta ya utalii baada ya kurekodi ongezeko kubwa la idadi ya watalii wa kigeni mwaka 2024. Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), jumla ya watalii 2,141,895 waliingia nchini, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.58 ikilinganishwa na mwaka 2023.

Hii ni mara tatu zaidi ya idadi ya watalii walioingia nchini mwaka 2020 wakati dunia ilipokumbwa na janga la Uviko-19, ambapo ni 620,867 pekee waliotembelea Tanzania.

Kwa upande wa miezi, Julai umeibuka kinara kwa kuvutia wageni wengi zaidi, huku watalii 218,065 wakiwasili nchini. Kinyume chake, Aprili ndiyo ilikuwa na idadi ndogo zaidi, ikiwa na watalii 116,280 pekee.

Ongezeko hili linaonyesha mvuto wa Tanzania kama kivutio cha utalii duniani, huku vivutio kama Hifadhi ya Serengeti, Mlima Kilimanjaro, na fukwe za Zanzibar vikichangia kwa kiasi kikubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks