Lissu: tutadai madadiliko kwa shuruti

January 29, 2025 5:48 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Ili kudai mabadiliko ya mfumo mpya wa uchaguzi nchini kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025

Dar es Salaam. Mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema watatumia njia ya shuruti ili kushinikiza mabadiliko ya mfumo mpya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2025.

Hata hivyo, Lissu amesema kutumia shuruti kudai mabadiliko si msimamo wa Chadema bali ni maoni yake binafsi.

Lissu aliyekuwa akizungumza na vyombo vya habari baada ya kupokelewa kwenye ofisi za makao makuu amesisitiza kuwa Chadema haitashiriki katika uchaguzi wowote ikiwa hakutakuwa na mageuzi ya mfumo wa uchaguzi, akilenga kuleta mabadiliko kwa njia za shuruti kama ilivyofanyika katika nchi za jirani.

“Tunazungumzia njia zisizo za kawaida za kufanya siasa, tunazungumzia njia za kushurutisha mageuzi, njia za kawaida ndio hizi za kwenda kupiga magoti wabadilike na kushiriki bila kujali hali…

…tunazungumzia kupata mageuzi kwa shuruti kama walivyopata Kenya, Malawi na Zambia, mnafikiri ilikuja hivi? Tunakwenda kutafuta mageuzi kwa shuruti, Bunge linaweza kukaa muda wote hata kama sio ratiba,” amesema Lissu.

Msimamo wa kutoshiriki uchaguzi ikiwa hakutakuwa na mageuzi ya mfumo wa uchaguzi unaojulikana kama ‘No Reform, No Election,’ (hakuna uchaguzi bila mabadiliko) umekuwepo hata kabla ya Lissu kushika hatamu.

Hata hivyo, tofauti na wakati uliopita, kauli ya Lissu anaashiria kuongezeka kwa  kiwango cha kudai mabadiliko hayo yatakayo shinikizwa kwa njia za shuruti, ambazo ameziita ni mikakati isiyo ya kawaida ya kisiasa.

Chadema, kama chama kikuu cha upinzani kwa muda mrefu kimekua kikikosoa mfumo wa uchaguzi wa Tanzania kwa madai ya ujanja, ufisadi, na kutokuwa na uwazi, kikidai kuwa mfumo huu hauwezi kutoa matokeo ya haki na ya kuaminika

Kwa muktadha wa kauli ya Lissu, ‘shuruti’ inaweza kumaanisha mbinu za kisiasa ambazo hazitegemei mazungumzo ya kawaida au mchakato wa kikatiba pekee. 

Badala yake, inaweza kuhusisha maandamano makubwa ya umma, kampeni za kuishinikiza mifumo na hata kushinikiza kwa njia za kisiasa na za kijamii ili kudai mabadiliko. 

Lissu ametaja mifano ya nchi kama Kenya, Malawi, na Zambia, ambapo mageuzi ya kisiasa na kikatiba yamefikiawa kwa njia za shuruti, ikiwemo maandamano na shinikizo la kimataifa.

“Tukifanya harakati sawasawa, tukifanya shuruti sawasawa, tutapata mageuzi na tutaenda kwenye uchaguzi kwa mfumo mpya wa uchaguzi, tukifanya kwa kujaribu hatutafika popote, kwahiyo nawaombeni tujiandae,” amesema.

Hata hivyo, Serikali imeanza kufanya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kuwa na mwelekeo wa kuimarisha demokrasia, ingawa vyama vya upinzani, hususan Chadema, haviyaungi mkono.

Baadhi ya mabadiliko muhimu yaliyofanyika ni ruhusa ya mikutano ya hadhara ya kisiasa iliyoruhusiwa kuanzia Januari 2023, baada ya katazo lililodumu kwa miaka takribani sita yakiviwezesha vyama vya upinzani kujieleza na kuwasilisha sera zao moja kwa moja kwa wananchi.

Jingine ni kuundwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) iliyoanzishwa ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi na haki, ikiwa na jukumu la kusimamia uchaguzi na kuhakikisha sheria za uchaguzi zinazingatiwa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
24 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
24 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
24 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Nukta TV

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Nukta TV

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Nukta TV