Polisi: Maandamano ya Chadema yalizuiwa kwa mujibu wa sheria

September 26, 2024 6:01 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Polisi yasema kulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani.
  • Yasisitiza kila haki ina wajibu unaotakiwa kufuatwa.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema lilizuia maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mujibu wa sheria kutokana na uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa amani na si kwa kukiuka sheria kama ilivyotafsiriwa na baadhi ya wadau wa sheria.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi iliyotolewa leo Septemba 26, 2024 kupitia kwa msemaji wake, David Misime, Jeshi la Polisi lina mamlaka kisheria kuzuia maandamano au mikutano ya kisiasa endapo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani. 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Sheria ya Vyama vya Siasa sura ya 258, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019, inaruhusu polisi kutoa zuio ikiwa mkutano au maandamano yanaonyesha dalili za kuvuruga amani au kuathiri usalama wa umma.

“Endapo mkutano au maandamano yanaonesha au yamedhamiriwa kusababisha uvunjifu wa amani au kuathiri usalama wa umma katika eneo hilo, Mkuu wa Polisi ambaye amepokea taarifa ya mkutano au maandamano hayo atatoa zuio la kufanyika kwa mkutano au maandamano hayo,” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha, Jeshi la Polisi limefafanua kuwa sababu za kuzuia maandamano ya Chadema zilitolewa kwa maandishi kwa mujibu wa sheria, na zilijumuisha matamshi ya viongozi na wafuasi wa chama hicho yaliyoashiria uwezekano wa kuvuruga amani.

Taarifa ya Jeshi la Polisi inakuja baada ya kuwepo na maoni tofauti kutoka kwa wadau mbalimbali wa sheria akiwemo rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Boniface Mwabukusi aliyehoji uhalali wa polisi kuzuia maandamano yanayoruhusiwa kisheria na lini litaruhusu maandamano hayo kufanyika baada ya jeshi hilo kupiga marufuku maandamano ya Chadema yaliyopangwa kufanyika Septemba 23, 2024.

Chadema iliitisha maandamano hayo kwa ajili ya kuomboleza kifo cha kada wao Ally Kibao pamoja na kuhimiza uwajibikaji serikalini kutokana uwepo wa vitendo vya utekaji na mauwaji ya watu ambapo pamoja na Jeshi la Polisi kuyapiga marufuku Chadema ilishikilia msimamo wa kuyafanya.

Septemba 23, 2024 Jeshi la Polisi liliwakamata wanachama 14 wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe kwa kukiuka amri halali ya polisi ambao waliachiwa siku hiyo hiyo usiku.

Kwa mujibu wa polisi licha ya haki ya kufanya maandamano kuainishwa kwenye Katiba ya Tanzania, haki hiyo imeambatana na wajibu wa kuhakikisha usalama na amani ya nchi inahifadhiwa.

Kwa upande mwingine, Jeshi la Polisi limeelekeza kuwa kama chama cha siasa hakikubaliani na zuio la maandamano, kinapaswa kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani kama inavyotakiwa na sheria, pia limesisitiza kuwa halitasubiri hali ya uvunjifu wa amani ijitokeze bali litachukua hatua za mapema ili kulinda usalama wa nchi.

Aidha, kuhusu lini itaruhusu kufanyika kwa maandamano hayo Jeshi la Polisi limesema sheria haimlazimishi Mkuu wa Polisi anayetoa zuio kueleza ni lini mkutano au maandamano yaliyozuiwa yanaweza kufanyika likisisitiza kuwa litaendelea kuchukua hatua stahiki kwa mtu, watu au kikundi cha watu, kiongozi wa chama cha siasa au wafuasi wao wanaopanga, wanaohamasisha au wanaotenda vitendo vya kihalifu vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

“Kamwe halitasubiri kuona moshi unafuka halafu liambiwe subiri moto uwake ndio lichukue hatua kwani kufuka kwa moshi ni kiashiria cha kuelekea kwenye kuwaka moto wa uvunjifu wa amani. Hivyo, Jeshi la Polisi litaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 5 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi wasaidizi kama ilivyorejewa mwaka 2002 ikiwemo kulinda amani ya nchi,” imesema taarifa ya polisi.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV