Polisi wazua mkutano wa Chadema na wanahabari Dar es Salaam

January 27, 2025 1:59 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Wazingira ofisi ya Chadema wakiwa na silaha na kuzuia watu kuingia ndani wakiwemo watumishi wa Chadema

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limezua kufanyika kwa mkutano baina ya waandishi wa habari na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika uliopangwa kufanyika leo Januari 27 kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho Mikocheni, Dar es Salaam.

Nukta habari imefika katika ofisi za hizo na kushuhudia askari polisi wakiwa wenye silaha wakiwa wametanda nje ya geti wakiwaamuru waandishi wote wa habari waliofika kwa ajili ya mkutano huo kuondoka.

Kwa mujibu wa Apolinali Boniface, Msaidizi wa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya nje wa Chadema, Jeshi la Polisi halijawapa taarifa yoyote ya sababu zilizopelekea kuzuiliwa kufanyika kwa mkutano huo.

“Wamepaki gari nje wanazuia mtu yeyote ambae unakuja ofisini, hata watumishi wa Chadema waliokuja baada ya wao kufika,” amesema Boniface.

Nukta Habari imefanya juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Jumanne Murilo ili kupata ufafanunuzi wa sababu za kuzuiwa kwa mkutano huo lakini simu yake imepokelewa na msaidizi wake aliyesema Murilo yupo kwenye kikao na atatoa taarifa juu ya zuio hilo.

Baadhi ya vyombo vya habari kikiwepo Jambo TV vimeainisha kuwa, huenda kuzuiliwa huku kunasababishwa na kuwepo kwa mkutano wa Kimataifa wa Nishati ‘Mission 300’ hivyo ungetakiwa kusogezwa mbele baada ya Januari 28 utakapomalizika.

Mkutano huo unahusisha wakuu cha nchi za Afrika na una malengo ya kujadili masuala ya nishati na maendeleo.

https://twitter.com/i/status/1883789755231699118
Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV