Kampuni tatu zaibuka kidedea Vodacom Digital Accelerator Tanzania Ni Afya Lead, Go Go App na Altit

July 12, 2024 8:09 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni Afya Lead, Go Go App na AltitudeX ambazo zitapata fursa zitakazofungua milango ya kupata mitaji na ushauri wa kitaalamu wa kukuza biashara. 

Dar es Salaam. Kampuni changa tatu zimeibuka kidedea katika mashindano ya Vodacom Digital Accelerator (VDA), hatua itakayo ziwezesha kupata fursa za mitaji yakukuza biashara zao pamoja na ushirikiano na kampuni mbalimbali za ndani na za kigeni.

VDA ni mpango unaotafuta waanzilishi wa kampuni changa wenye suluhisho la kiubunifu ili kutoa uwezeshaji na kupeleka biashara hizo kwenye ngazi inayofuata ya uzalishaji. 

Mpango huo wenye takribani miaka mitatu sasa unaendeshwa na  kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania na kampuni ya kukuza ubunifuni na biashara ya Smartlab.

Kampuni zilizoshinda shindano hilo ni Afya Lead iliyoibuka mshindi wa kwanza, GO GO app katika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na AltitudeX. 

Ushindi huo umekuja baada ya kampuni hizo zinazochipukia kupata mafunzo ya miezi mitatu na  kuwasilisha mpango kazi wenye manufaaa makubwa katika jamii

Kampuni hizo zilishinda shindano hilo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam Julai 11, 2024 ambapo washindani walipata nafasi ya kuwasilisha mawazo yao kuhusiana na makampuni yao na kuulizwa maswali ambayo yaliwasaidia kutetea mawazo yao na kuwafanya kuibuka washindi.


Soma zaidi:Ripoti: Afya ya akili chanzo cha watu kujiua, kuua Tanzania


Kampuni ya Afya Lead Ltd iliibuka kidedea baada ya kuonesha namna itakavyoleta mabadiliko chanya kwa wanawake wa Kitanzania wakati wa kujifungua kwa kupunguza kupoteza damu kwa wingi kupitia Mkanda Salama unaotumika kubana mshipa wa damu wa mwanamke aliyejifungua kwa njia ya kawaida.

“Nikiwa na miaka 13 nilimpoteza dada yangu wakati wa kujifungua kwa kukosa huduma nzuri za kiafya pamoja na vifaa vya kujifungulia baada ya kuvuja damu nyingi wakati wa kujifungua hivyo ikanibidi nipambane ili kuokoa maisha ya wanawake wengine,” amesema Frank Musa, ambaye ni mwanzilishi mwenza wa Afya Lead.  

Musa ameeleza kuwa Mkanda Salama utaenda kusaidia wanawake wengi zaidi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya yakiwemo mashirika ya nje kama Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ili kuokoa maisha ya wanawake wengi.Mjasiriamali huyo amesema mkanda huo ni rahisi kutumika na wanawake na gharama yake ni nafuu kwa kuwa unaweza kutumika na hadi watu watano. Hata hivyo, amesema bei halisi ya mkanda huo ni Sh 175,000 na huziuzia taasisi za huduma za afya. 

Wawakilishi wa kampuni ya Afya Lead, Go Go App na AltitudeX zilizotwaa ushindi katika mashindano ya Vodacom Digital Accelerator (VDA).Picha|VDA/X (Twitter).

Go Go App na dharura barabarani

Go Go App walioshika nafasi ya pili wao wanajihusisha utoaji huduma za msaada barabarani  kwa njia ya simu janja hususan masuala yanayohusu dharura za magari kama kupata pancha ama hitilafu nyingine yeyote kwenye vyombo hivyo vya moto.

Mwanzilishi wa Go Go App, Lusekeyo Nkuyi ameiambia Nukta Habari kuwa mtu mmoja au taasisi inaweza kupata huduma kutoka katika app na sasa wanazihudumia kampuni za simu, bima na watumiaji wa kawaida. 

“Huduma zetu ni kuanzia Sh5,000 hadi Sh10,000 kwa huduma ya kawaida lakini pia mtu anaweza kulipia ‘membership’ (uanachama) kwa mwaka Sh30,000 au kulipia kila mwezi Sh5,000 tu.

“Kwa watu wa bima huduma inakuwa ni bure kwa sababu atakuwa analipia moja kwa moja katika mfuko wake wa bima kupata huduma zetu… gharama inatofautiana kulingana na muda ulopata tatizo,” amesema Nkuyi. 

Huduma hiyo ya Go Go App kwa sasa inapatikana kwenye simu janja za Android na iOS. 

AltitudeX na vipimo vya kilimo kwa drone

Kampuni iliyoshika nafasi ya tatu AltituteX yenyewe inajihusisha na utoaji wa huduma utafiti wa kilimo kwa njia ya teknolojia ya kisasa inayotumia ndege nyuki (drone) kupima ardhi na mazao kwa mionzi kujua hali zake. 

Kupitia vipimo vinavyochukuliwa na drone hizo, wakulima wanaweza kupata majibu juu ya aina mbolea au dawa ya wadudu zinazohitajika kwa wakati huo.

“Mteja atatoa gharama ya Sh25,000 kwa huduma ila inapofika yeye kutaka kufanya umwagiliaji  au unyunyiziaji wa mbolea mteja atajigharamia kila kitu mwenyewe na sisi tukatoa tu hudumaa kwa gharama hiyo,” Rosi Funja mwanzilishi wa AltitudeX ameiambia Nukta Habari. 

Kwa mwaka huu, mashindano hayo yaliandaliwa na Vodacom Digital Accelerator kwa kushirikiana na MassChallenge pamoja na Huawei yamelenga kuchochea ukuaji wa kampuni changa kwa kutoa ushirikiano ambao huongeza mtandao wa kimataifa na utaalam katika kuongeza kasi ya uanzishaji na kuwapa washiriki wa VDA rasilimali muhimu na ushauri.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV