Watoto mapacha wafariki baada ya kutumbukia kwenye lambo la maji

April 25, 2023 12:52 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Lambo hilo la kunyweshea mifugo liko karibu na nyumba yao.
  • Polisi yawatupia lawama wazazi kwa kushindwa kuwalinda watoto.

Mwanza. Watoto wawili mapacha wenye umri wa mwaka mmoja na miezi sita wa familia moja wamefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye lambo la kunyweshea mifugo lililopo mita chache kutoka kwenye nyumba yao mkoani Mwanza huku uzembe ukitajwa kama sababu ya kugharimu uhai wao. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo April 25, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Wilbrod Mutafungwa amesema tukio hilo lilitokea Aprili 23 mwaka huu, majira ya saa 8:00 mchana katika Kijiji cha Runele, Kata ya Hungumalwa, Tarafa ya Nyamilama wilayani Kwimba Mkoa wa Mwanza.

Kamanda Mutafungwa amesema siku ya tukio watoto  hao wakiwa nyumbani peke yao bila uangalizi wa wazazi, walitoka kwenda kucheza nje kidogo na nyumbani kwao na kutumbukia kwenye lambo la maji lililopo jirani na nyumba yao umbali wa mita 30.

“Watoto hao mapacha wote wa jinsia ya kiume ambao wamefariki, siku hiyo wakiwa peke yao nyumbani kwa wazazi wao walitoka kwenda kucheza, bahati mbaya walitumbukia kwenye lambo la maji lililotengenezwa na wazazi wao ili kuhifadhi maji ya kunyweshea mifugo na shughuli zingine za kibinadamu,” amesema Kamanda Mutafungwa.

Mutafungwa amesema chanzo cha vifo vya watoto hao ni uzembe wa wazazi kutokuwa makini na watoto wao.

Wakati tukio linatokea mama yao alikuwa amekwenda kutafuta kuni na baba alikuwa akichunga mifugo, waliporudi hawakuwakuta watoto na kulazimika kuwatafuta bila mafanikio.

Wakati wakihangaika kuwasaka watoto wao wakishirikiana na majirani waliibaini miili yao ikiwa inaelea juu ya maji kwenye lambo, lakini tayari walikuwa wamepoteza maisha na miili hiyo imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu kwa mazishi.

Ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini na kutimiza wajibu na jukumu la msingi la malezi ya watoto wao ili kuwaepusha na madhara yanayoweza kujitokeza badala ya kuwaacha bila uangalizi wa watu wazima.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
28 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
28 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
28 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Jinsi afya ya akili inavyowatesa wanawake makazini

Jinsi afya ya akili inavyowatesa wanawake makazini

Nukta TV

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV