Polisi kuchunguza maiti za wanawake watatu zilizookotwa kando ya mto

January 20, 2022 6:07 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Miili yao imekutwa na majeraha kando ya mto uliopo Mtaa wa Mecco Kusini mkoani Mwanza.
  • Polisi yaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Dar es Salaam. Wanawake  watatu ambao bado  hawajatambulika  na wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 18 hadi 25  wamekutwa  wameuawa kando ya mto uliopo nyuma ya kituo cha afya Buzuruga katika mtaa wa  Mecco Kusini mkoani Mwanza.

Wakizungumza kwenye eneo la tukio baadhi ya mashuhuda wamesema wameshuhudia miili hiyo ikiwa utupu ikiwa na majereha mbalimbali kabla  ya kuchukuliwa na askari polisi na kuihifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Seokoture mkoani hapa.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mecco,  Scholastica Barnabas amesema ameshuhudia tukio hilo jana Januari 19, 2022 majira ya saa 7 mchana na kukutana miili ya watu hao ikiwa utupu.

“Baada ya kuona tukio hilo nilimpigia Mkuu wa Polisi  Wilaya  ya Ilemela (OSC) kuja kufuatilia tukio hilo,” amesema  Scholastica.

Shuhuda mwingine Japhet Mabula ameviomba vyombo vya usalama kufanya uchunguzi na kuimarisha usalama mkoani humo.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza,Gidion Msuya  amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana  kwenye mto uliopo nyuma ya kituo cha mabasi Buzuruga wilayani Ilemela. 

Amesema watu hao hawajafahamika majina na sehemu wanakoishi na kwamba uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha tukio hilo. 

“Chanzo cha tukio la mauaji hayo hakijafahamika,  tunaendelea kuchunguza ingawa marehemu wamekutwa wakiwa na majereha sehemu mbalimbali za miili yao, ” amesema Msuya.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW