Kutana na App inayokurejeshea ‘password’ ya simu uliyosahau
- Inakutunzia neno la siri na kukumbusha kama umesahau wakati ukitumia simu yako.
- Siyo rahisi kudukuliwa wala kuingiliwa na wahalifu.
- Pia inatumika katika utunzaji wa nyaraka muhimu mtandaoni.
Huenda wewe ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakisahau neno la siri (Password) la simu yako au mitandao ya kijamii mara kwa mara, jambo linalokuletea usumbufu wa kuifungua upya na kujikuta ukipoteza baadhi ya vitu muhimu.
Basi suluhisho limepatikana, kwa kutumia programu tumishi ya Dashlane iliyotengenezwa na kampuni za Google na Apple unaweza kudhibiti maneno ya siri yote za simu yako kwa kuhakikisha neno lililosahaulika linarejeshwa.
Siyo tu inakukumbusha na kukuwekea neno la siri la kuingilia kwenye simu yako kama umesahau, bali inahakikisha neno unalotumia linakua imara na salama.
Utendaji wa App hiyo unatumia mfumo wa usanifu wa maarifa sifuri (Zero Knowledge Architecture) ambapo unatengeneza neno la siri kuu ambalo linatunzwa nje ya mtandao ambapo siyo rahisi kudukuliwa au kufahamika hata kwa Wahandisi wanaosimamia app hiyo.
Soma zaidi:
- Mfahamu GIven Edward, mtanzania aliyeshinda tuzo mbili za kimataifa katika sekta ya elimu
- Apps za elimu zinazoweza kuwaelimisha watoto wadogo kabla ya kwenda shule
Hata kama umedukuliwa mtandaoni, Dashlane inakujulisha mara moja kubadili neno la siri la simu, kompyuta na mitandao unayotumia ili kujiweka salama zaidi.
Unaweza pia kuitumia Dashlane katika shughuli za utunzaji wa nyaraka kwenye vifaa vingine kama kompyuta ikiwemo taarifa za risiti za mauzo, usafirishaji na hata kadi za manunuzi mtandaoni.
App hiyo yenye watumiaji zaidi ya milioni 10 inapatikana bila malipo yoyote lakini changamoto yake ni kuwa haiwezi kufungamanishwa na barua pepe zaidi ya moja.