Wanafunzi 46,838 mwaka wa kwanza wapata mikopo elimu ya juu 2019-2020

November 11, 2019 4:34 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu, waliyohudhuria katika Baraza la Maulid ya Mtume Muhammad, lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Benki Kuu, jijini Mwanza, Novemba 10, 2019. Picha|Ofisi ya Waziri Mkuu.


  • Idadi ya wanafunzi waliopata mikopo ni hadi kufikia Novemba 3, 2019.
  • Fedha hizo ni sehemu ya Sh450 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu.
  • Serikali yasema inaendelea kufanyia kazi maoni na mapendekezo ya wadau mbalimbali ili kuboresha mfumo wa utoaji mikopo ya elimu ya juu.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia Novemba 3 mwaka huu, Serikali imetoa mikopo ya Sh162.8 bilioni kwa wanafunzi 46,838 wa mwaka wa kwanza ili kuwawezesha kumudu gharama za masomo kwa mwaka 2019/2020.

Majaliwa ametoa taarifa hiyo Novemba 10, 2019 wakati akizungumza na maelfu ya waumini waliohudhuria Baraza la Maulid kitaifa katika viwanja vya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Capripoint, jijini Mwanza.

“Kwa mwaka 2019/2020, Serikali imetenga jumla ya Sh450 bilioni kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi walengwa 128,285. Na hadi tarehe 3 Novemba, 2019 wanafunzi 46,838 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka 2019/2020, walikuwa wamepewa mikopo inayofikia Sh162.8i bilioni,” amesema.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais John Magufuli, amesema Serikali inatambua kuwa utoaji wa huduma ya elimu ni gharama na kuwa baadhi ya wananchi hawawezi kumudu gharama hizo, hivyo ikaamua kuanzisha utaratibu wa kutoa mikopo ya elimu ya juu kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (Heslb)

 “Mikopo inayotolewa na Serikali, huongozwa na Sheria ya Bodi ya Mikopo (Sura 178) inayotaja vigezo vya wahitaji na wenye udahili lakini wasio na uwezo wa kumudu gharama zote au sehemu ya gharama za mafunzo au kwenye maeneo ya kipaumbele ikiwemo yatima na wanaotoka familia zenye kipato duni,” amesema Majaliwa katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu. 


Zinazohusiana


Hata hivyo, amesema Serikali inaendelea kufanyia kazi maoni na mapendekezo ya wadau mbalimbali ili kuboresha mfumo wa utoaji mikopo ya elimu ya juu. 

Katika mwaka wa fedha wa 2019/2020, Serikali imetenga Sh450 bilioni kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu, ikiwa imeongezeka kutoka Sh427 bilioni zilizotengwa mwaka uliopita.

Mwaka huu, Heslb ilipokea jumla ya maombi 87,747 ambapo kati ya maombi hayo, ni maombi 82,043 sawa na asilimia 93.4 yalikuwa yamekidhi vigezo vya maombi. 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Heslb, Abdul-Razak Badru aliyekuwa akizungumza na wanahabari leo (Oktoba 17, 2019) alisema utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu inatolewa kwa awamu kulingana na orodha ya wadahiliwa ya vyuo vikuu inayotolewa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Mikopo hiyo husaidia wanafunzi kuweza kumudu gharama za masomo na maisha wakati akisaka elimu hiyo ya juu.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV