Bajeti bodi ya mikopo yaongezwa kwa asilimia 14.7, wanafunzi wakikata rufaa

November 21, 2022 12:51 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Imeongezeka hadi kufikia Sh654 bilioni mwaka 2022/23.
  • Sh84 bilioni kuwanufaisha wanafunzi 28,000 walikosa mikopo.
  • HESLB yapokea rufaa za wanafunzi. 

Dar es Salaam. Huenda wanafunzi 28,000 waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali watapata ahueni baada ya Serikali kuongeza bajeti ili kuwawezesha kupata mikopo kugharamia masomo ya elimu ya juu.

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania (HESLB) imeongezewa bajeti ya Sh84 bilioni ikilinganishwa na Sh570 bilioni zilizotengwa awali kwa ajili ya mwaka wa masomo wa 2022/23.

Hilo ni sawa na ongezeko la asilimia 14.7 ambapo sasa bajeti ya mikopo ya elimu ya juu imefikia Sh654 bilioni.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema nyongeza hiyo ya Sh84 bilioni itawezesha wanafunzi 28,000 kupata mikopo kwa robo ya kwanza ya mwaka wa masomo na tayari fedha hizo zimeshafikishwa katika vyuo husika.

 Wanafunzi hao licha ya kuwa na sifa walikosa mikopo kutokana na bajeti iliyopangwa kutokukidhi mahitaji ya wanafunzi waliokuwa na difa ya kupata mikopo hiyo. 

 “Bajeti isingeongezwa ni wazi wanafunzi 28,000 wangekosa mikopo lakini kutokana na hatua hii iliyochukuliwa wataweza kupata ufadhili huu. Hawa waliopata walikuwa tayari wameshafanyiwa tathmini na kuonekana mahitaji yao ni makubwa,” amesema Badru.


Soma zaidi:


Kwa mujibu wa Badru, hadi kufikia leo jumla ya wanafunzi 166,438 wamepangiwa mikopo yenye thamani ya Sh424.5 bilioni. Kati yao wa mwaka wa kwanza ni 68,460. 

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaolengwa kunufaika na mikopo hiyo kwa mwaka huu ni 71,000.

 

Waliokata rufaa

HESLB imepokea rufaa 32,777 za wanafunzi wahitaji wa mikopo ya elimu ya juu waliowasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia dirisha la rufaa lililofungwa jana Jumapili (Novemba 20, 2022).

Rufaa hizo ni maombi yaliyowasilishwa na wanafunzi wahitaji kutokana na kutoridhishwa na viwango vya mikopo waliyopangiwa na HESLB katika awamu mbalimbali za upangaji na utoaji mikopo katika mwaka wa masomo 2022/23

Badru amesema majibu ya rufaa hizo yatatangazwa Jumamosi Novemba 26, 2022 na wanafunzi watapata taarifa za kina katika akaunti walizotumia kuomba mkopo maarufu kama SiPA (Student’s Individual Permanent Account).

“HESLB inaendelea kupanga mikopo kwa wanafunzi wote wahitaji na kwa wale wanaoendelea na masomo tunavisisitiza vyuo kuendelea kutuma matokeo ya wanafunzi……Tumeendelea kupeleka fedha katika vyuo mbalimbali nchini,” amesema Badru.

HESLB imewataka waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa kupitia rufaa ukiendelea na wale waliopangiwa mikopo, taarifa zao zinapatikana kwenye SiPA na fedha zao tayari zimeshatumwa vyuoni.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV