Filamu ya “Bad Boys for Life” kuwarudisha Smith na Lawrence ulingoni

January 17, 2020 11:53 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

Kauli ya Burnett anaposema “inatosha Mike, ninahitaji kustaafu” inaumiza moyo wa Smith ambaye maisha yake yote ya kazi amefanya akiwa na rafiki yake huyo kipenzi. Picha| Mtandao.


  • Ni mwendelezo wa filamu za “Bad Boys for Life” ambapo ya kwanza ilitoka miaka ya 1990.
  • Inasimulia kisa cha marafiki wawili waliokula kiapo cha kuwa pamoja maisha yao yote.
  • Inafundisha urafiki pamoja na umuhimu wa kufanya maamuzi.

Dar es Salaam. Baada ya kumuona Will Smith akitamba kwa mwaka jana, muigizaji huyo ameanza mwaka 2020 akishirikiana na mkongwe Martin Lawrence kuirudishia uhai wa filamu ambayo imetoka kwa mara ya kwanza mwaka 1995.

Ni filamu ya “Bad Boys for Life” ambayo inafikisha sehemu tatu leo Januari 17, 2020 baada ya kungia rasmi kwenye kumbi za sinema, inasimulia kisa cha marafiki wawili waliokula kiapo cha kuwa pamoja maisha yao yote.

Askari mpelelezi Mike Lowrey (Smith) na mwenzake Marcus Burnett (Lawrence) wamefanya kazi nyingi sana pamoja. Kukamata majasusi wakubwa na kufichua kesi nyingi ambazo wahalifu walifikiria wamefyeka kila aina ya ushahidi, haikuwa jambo geni kwenye kazi zao.

Kauli ya Burnett anaposema “inatosha Mike, ninahitaji kustaafu” inaumiza moyo wa Smith ambaye maisha yake yote ya kazi amefanya akiwa na rafiki yake huyo kipenzi.


Zinazohusiana


Mambo yanabadilika kabisa kwa Smith baada ya rafiki yake kuchagua kuoa na kustaafu, analazimika kufanya kazi peke yake.

Mbali na kuua kwa kupitiliza kwenye “mission” ambazo anafanya, Lowrey anakosa furaha na kazi yake. 

Mambo yanazidi kusogea kwenye “chorus” baada ya kazi moja kuhitaji uwepo wa Burnett kwani bila yeye, haiwezi kwenda sawa.

Unahitaji kutazama jinsi risasi zinavyofyatuka kuimarisha hali ya usalama na zaidi kazi yako inaweza kukupatia rafiki wa maisha.

Filamu hii iliyogharimu Sh207.1 bilioni imesimamiwa na kiongozi Bilall Fallah aliyeongoza filamu ya Image 2014 akishirikiana na Adil El Arbi imehusisha mastaa wengine wakiwemo Vanessa Hudges na Alexander Ludwig.

Unaweza kuitazama kwa njia ya mtandao au kuangalia kwenye kumbi za kuangalizia filamu zikiwemo za Century Cinemax. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV