Furahia wikiendi yako na filamu ya daktari anayeongea na wanyama

January 11, 2020 6:36 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Imesheheni wakongwe wa tasnia ya uigizaji wakiwemo Iron Man na John Cena.
  • Inasimulia kisa cha daktari anayeweza kuongea na wanyama.
  • Kama umefurahia “Maleficent” na “Jumanji”, hii pia haitokula pesa yako bure.

Dar es Salaam. Ndiyo kuanza mwanzo wa mwaka na huenda hii ndiyo wikiendi yako ya pili kama haukututangulia kuingia mwaka 2020. Laa, ni masihara tu!

Hata hivyo, bado una nafasi kubwa ya kuwa na nguvu na kuendelea kufurahi kwa sababu vijana wa kizazi kipya wanaishi kwa msemo wa “YOLO” (You Only Live Once) kwa maana ya kwamba una nafasi moja tu ya kuishi hivyo ni kwa nini “usivunje mifupa kama meno yapo”?

Kama wewe kuvunja kwako mifupa ni kwa kuangalia filamu basi ni hakika utafurahia kile ambacho kampuni ya kuonyesha filamu nchini ya Century Cinemax imekuandalia kwa wikiendi hii ya “Doctor Dolittle

Filamu hii imeigizwa hapo awali na mwigizaji Eddie Murphy lakini kwa mwaka 2020, msanii ambaye kila mtoto anatamani kuwa na nguvu zake yaani “Iron Man” Robert Downey ameshikilia usukani wake.

Akiungana na waigizaji pamoja na sura maarufu zikiwemo za John Cena na Emma Thomson, Downey anasimulia kisa cha kufikirika kinachomuhusu daktari ambaye ana uwezo wa kuongea na wanyama.


Zinazohusiana


Ndiyo. Kumsikia kasuku sio tija kwake kwani yeye anaweza kuongea na samaki na pweza wa baharini. Unadhani ameishia hapo? Daktari huyu anaelewana na nyangumi, sokwe na kila kitu kijulikanacho kama mnyama au ndege.

Hata hivyo masimulizi haya yasingeweza kufaa kama hatuwezi kuona ugomvi na ndipo safari inaanza baada ya baadhi ya vijana kuvuka mipaka isiyowahusu.

Hata hivyo, daktari huyu analazimika kutafuta tiba ya malkia Elizabeth pale anapougua kiasi cha kukosa tiba.

He’s just not a people person. @RobertDowneyJr is Dolittle.
Watch the trailer for #DolittleMovie in theaters January 2020 and ❤ this Tweet to get monthly updates. pic.twitter.com/UT2cgiMb1H

Safari yake inajaa misukosuko lakini hakika hautahitaji kukosa kuifuatilia na kusikia filamu hii ambayo hata msanii Selena Gomez anahusika.

Chini ya kiongozi Stephen Gaghan aliyeongoza filamu ya “Maleficent” na zingine kibao, filamu hii imegharimu kiasi cha Sh402.7 bilioni.

Utaweza kuiangalia kwenye skrini ambayo Century Cinemax wanadai ni kubwa kuliko zote Afrika Mashariki kwa Sh10,000 tu.

Enable Notifications OK No thanks