Mbinu za kufungua simu ya iPhone yenye “Face ID” ukiwa umevaa barakoa

May 21, 2020 6:35 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Tumia mfumo wa endeshi mpya wa simu za iPhone wa  iOS 13.5.
  • Mfumo huo unakupa urahisi wa kuifungua mara moja tu kwa kuweka neno siri.
  • Kama “Face ID” inakupa shida weka pembeni tumia njia nyingine za kufungua simu.

Dar es Salaam. Bila shaka janga la Corona limeleta athari nyingi siyo tu kuharibu uchumi wa dunia hata matumizi ya vifaa vya kielektroniki zikiwemo simu za mkononi. 

Kwa sasa watumiaji wa simu za iPhone za toleo la iPgoneX na kuendelea wanapata changamoto ya kufungua simu zao hasa wakiwa wamevaa barakoa. 

Simu hizo hufunguliwa kwa kuskani sura (Face ID) huhitaji kuskani macho, pua na mdomo ili uweze kuzifungua na kuendelea kuzitumia endapo zimelokiwa au kujiloki.

Hiyo ina maana kuwa ukiwa umevaa barakoa huwezi kufungua simu yako kwa kuskani sura kwa sababu mdomo na pua vitakuwa vimefunikwa na simu haiwezi kutambua barakoa na haitafunguka. 

Kutokana na kujikinga dhidi ya virusi vya Corona, baadhi ya watu hulazimika kuvaa barakoa wakati wote, jambo linalowaletea changamoto wakati kutumia simu zao za iPhone zenye mfumo huo. 

Lakini usihofu kila changamoto ina suluhu yake. Unawezaje kuifungua simu yako mara moja na ukiwa umevaa barakoa?

Simu hizo hufunguliwa kwa kuskani sura (Face ID) huhitaji kuskani macho, pua na mdomo ili uweze kuzifungua na kuendelea kuzitumia endapo zimelokiwa au kujiloki. Picha| Apple Support.

Ni rahisi, kufuatia mfumo endeshi mpya wa simu za iPhone wa  iOS 13.5 sasa mtu anaweza kufungua simu yake bila haja ya kulazimika kucheza na sura yake mara kadhaa.

Kwa sasa, mtumiaji wa simu za iPhone (X, XS, XS Max, XR, 11, 11 Pro na 11 Pro Max) anaposkani sura yake mara moja, anaweza kupangusa simu yake kutoka chini kwenda juu (Slide up) na atapata nafasi ya kuingiza neno siri “pin” yake moja kwa moja.

Hata hivyo itakuhitaji kusasisha (Update) programu yako kuwa iOS 13.5 ili kufanya hivyo.

Hauna haja ya kuvuta chini barakoa yako unapotaka kutumia simu yako kwenye mkusanyiko wa watu kwani inaondoa maana nzima ya wewe kuvaa barakoa kama utakuwa unavua mara kwa mara.


Zinazohusiana


Kwa sasa, baada ya kuwasha simu yako unaweza kupangusa kuelekea juu bila haja ya kuskani uso wako kuifikia sehemu ya kuweka neno siri kwa ajili ya kuifungua simu yako.

Njia nyingine unayoweza kuitumia ni kuzima huduma hiyo ya Face ID kama unaona muda mwingi unautumia ukiwa umevaa barakoa.

Nenda kwenye mpangilio wa simu yako na kisha ingia kwenye sehemu ya matengenezo (settings) na kisha chagua sehemu ya “Face ID na Passcode” na zima sehemu ya “Iphone unlock” baada ya hapo, utapangusa kuelekea juu ukiwasha simu yako.

Njia hizi zitakusaidia kutumia simu yako kwa uhuru na kukupunguzia muda unaotumia kuifungua.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW