Sifa za simu mpya ya Apple itakayozinduliwa Aprili 24

April 23, 2020 11:50 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni simu ya iPhone SE ambayo imejaa sifa lukuki.
  • Mbali na kurudia mfumo wa kamera moja, iphone SE inatambulishwa kuwa simu yenye kasi zaidi kwenye ulimwengu wa simu janja.
  • Bei yake ya kuanzia ni chini ya  Sh1 milioni.

Dar es Salaam. Kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya Apple ya Marekani inaendelea kuongeza ushindani katika biashara ya simu za mkononi duniani baada ya kuwaletea wateja wao “simu yenye kasi kuliko zote kuwahi kutokea.”

Simu hiyo ambayo ni iPhone SE inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho Aprili 24, 2020.

Kwa mujibu wa Apple kupitia tovuti yake, iphone SE ni simu itakayompatia mtumiaji wa simu za iPhone sababu zote za kuhamia kwenye simu hiyo huku ikivimba kifua kwa kusema ni simu ambayo kila mtu amekuwa akiisubiria. Ni nini kipya?

Kasi ya utendaji kazi

Kama simu yako ya sasa ina mwendo wa konokono, simu ya iphone SE ni ya aina yake kwani inatumia “chip” ya simu kama iliyotumika kwenye simu zake za iPhone 11 na iPhone 11 Pro, yaani teknolojia ya A13 Bionic ambayo inafanya utendaji kazi wa simu kuwa wa kugusa.

Hivyo ni kusema, mtumiaji wa simu hiyo anaweza kucheza michezo ya simu bila kuathiri kasi ya simu yake na hana haja ya kusubiri kwa sekunde kadhaa anapoiamuru simu yake kufanya kitu fulani.

“iPhone SE inafanya kupiga picha, kucheza michezo ya simu na pia uzoefu wa matumizi ya AR (kutazama ulimwengu halisi kwa njia ya picha za kidijitali) kuwa mtelezo kupitia teknolojia yake ya A13 Bionic,” imesomeka taarifa ya Apple.

“Touch id” iliyo kwenye kitufe cha mbele “home button” inaweza kutumika kwenye kufungua simu na kulinda programu tumishi zingine kwenye simu hiyo inayopatikana kwa rangi tatu ambazo ni nyeupe, nyekundu na nyeusi. Picha| Giphy.

Mtazamo mpya wa camera

Huenda haukufurahia macho matatu nyuma ya simu yako. iPhone SE imerudia mfumo maarufu wa kamera moja huku sifa yake ya picha za mfumo wa “Potrait” kutoka kwenye kamera ya megapixel 12. 

Kwa mujibu wa wadau wa teknolijia wa Tekno kona, MegaPixel (MP) ni mkusanyiko wa Pixel milioni moja huku Pixel ikiwa ni viboksi vidogo ambayo vinatumika katika kuijenga picha mpaka ikawa kwenye muonekano wake.

Zaidi, picha za “potrait” zinapatikana kwenye kamera ya mbele na nyuma.

Hata hivyo, kamera hiyo ambayo megapixel zake ni sawa na simu ya iPhone 11 pro ya Septemba 20, 2019 inasemekana kuwa bora zaidi kuliko simu zote za iPhone zenye kamera moja huku uwezo wake wa kupiga picha zenye kivuli na mwanga ukiwa kwa mfumo unaoonyesha picha kwa ubora wa aina yake yani HDR.


Zinazohusiana


Usalama

Taarifa ya kampuni hiyo imeainisha kuwa teknolojia ye “Touch id” iliyo kwenye kitufe cha mbele “home button” inaweza kutumika kwenye kufungua simu na hata kulinda programu tumishi zingine kwenye simu hiyo inayopatikana kwa rangi tatu ambazo ni nyeupe, nyekundu na nyeusi.

Zaidi, kivinjari cha Safari kinachotumika na simu za iPhone kinaendelea kuwa cha kipekee kwa kuzuia matangazo ya mtandaoni ambayo yamekuwa kero kwa watumiaji wa simu janja.

Simu hiyo inapatikana kwa gharama ya kuanzia Sh923,325 kwa simu yenye uhifadhi wa kumbukumbu wa GB64 huku yenye uhifadhi wa GB256 ikigharimu Sh1.3 milioni na hivyo kuwa simu ya bei ya chini ambayo imetolewa tangu simu za iPhone 11 zizinduliwe ambapo iPhone 11 yenye uhifadhi wa GB64 inagharimu Sh1.6 milioni.

Enable Notifications OK No thanks