WHO: Mbu hawaenezi virusi vya Corona

June 8, 2020 8:55 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Shirika hilo limesema hakuna taarifa wala ushahidi kuthibitisha dhana hiyo. 
  • COVID-19 ni ugonjwa wa mfumo wa upumuaji unaotokana na maji maji wakati kupiga chafya au kukohoa. 
  • Kunawa mikono na kuvaa barakoa ndiyo kinga. 

Dar es Salaam. Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wanaamini ugonjwa wa virusi vya Corona unaenezwa na mbu, basi unajidanganya kwa sababu dhana hiyo haina ukweli wowote. 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema mpaka sasa hakuna taarifa wala uthibitisho unaoelezea kuwa virusi vya COVI-19 vinaweza kuenezwa kwa mbu.

Mbu ambao hung’ata wakati wa usiku hueneza ugonjwa wa malaria ambao kwa sasa ndiyo unaua watu wengi zaidi duniani. 

WHO imesema COVID-19 ni ugonjwa wa mfumo wa upumuaji ambapo maambukizi yake hutokea kwa maji maji yanayotoka mdomoni au puani kwa mtu mwenye ugonjwa huo.


Zinazohusiana.


Kwa kawaida maji maji hayo yanaweza kwenda kwa mtu mwingine kupitia kupiga chafya au kukohoa au kugusa mahali ambapo mtu mwenye ugonjwa huo alipigia chafya au kukoholea. 

“Epuka kukaa karibu na mtu yeyote anayekohoa na kupiga chafya,” imeeleza WHO kama njia ya kuepuka maambukizi ya COVID-19.

Njia nyingine ni kutumia vitakasa mikono (sanitizers) na kuosha mikono kwa sabuni na maji tiririka lakini kuvaa barakoa kila unapokwenda katika mikusanyiko ya watu. 

Kumbuka kuendelea kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo ya wataalam wa afya kwa sababu Corona bado ipo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV