Ni uzushi: Kupiga mbizi kwenye maji hakusababishi Corona

December 4, 2020 10:44 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Bado haijathibitishwa kisayansi kwamba maeneo ya kuogelea ni njia ya mtu kupata Corona. 
  • Unashauriwa kuendelea kuchukua tahari ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara.

Dar es Salaam. Licha ya kuwa kuogelea (kupiga mbizi) kwenye mabwawa au baharini ni moja ya burudani inayoweza kumfanya mtu ajisikie vizuri, baadhi ya watu wameacha kuogelea kwa kuogopa kupata maambukizi ya COVID-19. 

Hata hivyo, dhana hiyo ambayo inalenga kuleta taharuki kwa watu, haina ukweli wowote kwa sababu bado haijathibitishwa kisayansi. 

Maeneo ya kuogelea siyo njia ya moja kwa moja kumsababishia mtu kupata COVID-19 ikizingitiwa kuwa ugonjwa huo unaenezwa kwa njia ya kugusana au kugusa maji maji yanayotokana na kikohozi au chafya ya mtu mwenye virusi hivyo. 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limewatoa hofu watu wanoapenda kuogelea na kuwataka kuendelea kupata burudani hiyo huku wakichukua tahadhari zinazohitajika kujikinga na ugonjwa huo.


Soma zaidi:


Tahadhari ambazo zinapendekezwa ni kukaa umbali wa mita moja kutoka mtu mmoja na mwingine, jambo ambalo linaweza kuzingatiwa na waogeleaji. 

Nyingine ni kuvaa barakoa, kutumia tishu wakati wa kukohoa au kupiga chafya na kunawa mikono kwa maji tiririka mara kwa mara. 

“Virusi vya Corona havisambazwi kwa maji unapoogelea. Hata hivyo virusi husambaa mtu anaposegea karibu na mtu mwenye Corona,” WHO inaeleza katika moja ya miongozo ya kudhibiti ugonjwa huo. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV